dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 8, 2016

KHUTBA YA KUAGA YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

Image result for images of islam
  • Khutba hii ilitolewa na Mtume Muhammad (SAW) tarehe 09 Dhul Hijja mwaka wa 10 Hijriya kwenye Mlima Arafah.
1. "Enyi watu! Nisikilizeni maneno yangu vizuri , kwani sidhani kama baada ya mwaka huu nitakuwa pamoja nanyi. Hivyo sikilizeni
kwa makini nitakayoyasema na (maneno haya ) mfikishieni kila
asiekuwepo hapa leo.

2. "Enyi watu! Hakika damu zenu na mali zenu ni takatifu kwenu kama mlivyoufanya mwezi huu kuwa mtakatifu na mji huu kuwa
mtukufu? rudisheni amana mlizokabidhiwa kwa wenyewe wanaostahiki.
Msimdhuru yeyote ili nanyi msije msije mkadhuriwa. Kumbukeni mtakuja
kukutana na mola wenu naye atahesabu amali zenu. Allah (SWT) amekukatazeni kula riba . Hivyo riba zote zimeondoshwa na mna haki ya kubaki na rasilmali (mitaji) yenu. Hamna haki ya kudhulumu wala kudhulumiwa . Allah(SWT) ameharamisha riba na kila haki ya kisasi iliyekuwepo enzi za Ujahiliya imefutwa!

3. "Enyi watu! washirikina wanajaribu kuakhirisha (kuchelewesha)
kalenda ili wafanye kuwa sawa idadi ya ile (miezi) aliyo
itukuza Allah na kulifanya halali jambo ambalo Allah(SWT) ameliharamisha
na kulikataza jambo ambalo Allah(SWT) ameliruhusu Miezi kwa Allah(SWT) ni
kumi na miwili. Minne kati yao ni mitakatifu, mitatu ikiambatana (Dhul Qaadah, Dhul Hijjah na Muharram) na mmoja (Rajab) uko kati ya Jumada (ya mwanzo na ya mwisho) na Shaaban.

4. "Jiepusheni na shetani kwa ajili ya kuilinda dini yenu . Tayari (shetani) amekata tamaa kwamba hataweza kuabudiwa katika ardhi hii milele lakini bado ana mikakati ya kukupotezeni hivyo
tahadharini nae katika mambo mengine."

5. "Enyi watu! ni kweli mna haki juu ya wanawake na wao pia wana haki juu yenu . Kumbukeni mmewachukua kuwafanya wake zenu kwa amana ya Allah(SWT) na mmehalalishiwa (kustarehe) nao.

6. "Nnakuusieni kuwatendea wema wanawake na kuwa na huruma kwao
kwani ni wake zenu ni wasaidizi wenu.

7. " Enyi watu, nisikilizeni kwa utulivu , mcheni Allah(SWT), msali sala tano kila siku, fungeni katika mfungo wa Ramadhan na toeni Zakah. Tekelezeni ibada ya Hijjah ikiwa mna uwezo."

8. "Binadamu wote wametokana na Adam na Hawaa, hakuna mbora kati
ya mwarabu na asiyekuwa mwarabu , wala asiekuwa mwarabu kwa
mwarabu, wala mweupe kwa mweusi au mweusi kwa mweupe
isipokuwa kwa Taqwa( kumcha Allah).*

9. "Enyi watu Eleweni * kila muislamu ni ndugu kwa muislamu na waislamu wote
ni ndugu. Hatohalalishiwa muislamu kitu chochote isipokuwa kile alichopewa kwa ridhaa na ndugu yake. Wala msidhulumu nafsi zenu. Na msisahau kwamba kuna siku mtakutana na mola wenu na
mtahesabiwa amali zenu. Hivyo tahadharini msije mkapotea baada
yangu"

10. "Enyi watu! Hakuna tena Mtume baada yangu na hakuna dini nyengine itakayokuja. Ninakuachieni vitu viwili ambavyo
mkishikamana navyo hamtopotea milele navyo ni QURAAN na SUNNA.

11. "Wale wote walionisikiliza waufikishe ujumbe huu kwa wengine
na wengine waufikishe kwa watakaofuatia na inawezekana hawa wa mwisho wakayafahamu vyema maneno yangu kuliko hawa walionisikiliza moja kwa moja."

"Ewe mola shuhudia kwamba nimefikisha ujumbe kwa watu wako".

No comments :

Post a Comment