Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Saturday, November 26, 2016

Afrika yamuomboleza Fidel Castro!

 

Taarifa ya kifo cha Fidel Castro imeibua hisia za majonzi na ushirikiano katika maeneo mengi Afrika .
Alikuwa mtu aliyekuwa mfano wa kuigwa katika harakati za baada ya uhuru kote barani kwamba wakati mmoja alijielezea kama "sababu nzuri zaidi ya kuwepo kwa binadamu ".

Uhusiano wake wa karibu hususan na taifa la Afrika kusini - na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi -umekuwa ukiheshimiwa kwa kiasi kikubwa.

Asakari wengi wa Cuba walipoteza maisha yao mbali na nchi yao katika nchi kama vile Angola, wakipigana vita vya ukombozi wa Afrika. Baadhi watadai kwamba katika siku ya leo wakati mmoja wa watu muhimu katika kane ya 20 hayupo tena, wanapaswa kukumbukwa pia.

Wakati usaidizi wa kimataifa katika kukabiliana na mlipuko wa Ebola katika mataifa ya magharibi mwa Afrika , Fidel Castro, aliahidi na kutuma takriban madaktari 300 wa ziada na wauguzi katika mataifa hayo.

Pia alisema kuwa Cuba iko tayari kusaidiana na Marekani katika masuala ya maslahi ya amani ya dunia.

Tangazo hilo lilitolewa baada ya rais Obama kuwataka Wamarekani kuepuka kupotosha ukweli juu ya Ebola.

Katika kipindi cha miongo kadhaa, Castro alituma madaktari wa Cuba katika nchi za kigeni kuwatibu maskini wakiwemo wakazi wa bara la Afrika.

Mbali na Matibabu mapenzi ya Castrol kwa Afrika yalidhihirika kusini mwa Afrika pale ilipoingilia katika katika vita vya Angolasuala lililobadili sababu ya historia.

Binafsi Castro aliongoza harakati za kivita katika Cuito Cuanavale manamo mwaka 1988 ambapo majeshi ya Cuba yalishinda jeshi la Afrika Kusini na matokeo yake majeshi ya Afrika Kusini hayakuondoka Angola pekee bali Namibia pia ilifanikiwa kupata uhuru wake.

Nelson Mandela binafsi alisema kuachiliwa kwake kutoka gerezani na kushindwa kwa ubaguzi wa rangi kulitokana na matukio ya Cuito Cuanavale.

/Muungwana

No comments :

Post a Comment