dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 5, 2016

Mnigeria Ateuliwa Katika Bodi ya Washauri wa Uchumi wa Donald Trump!

 RAIS mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mfanyabiashara raia wa Nigeria, Adebayo Ogunlesi (pichani juu), kuwa mmojawapo katika bodi ya washauri wake wa masuala ya uchumi.

Tovuti ya Business Insider imeeleza kuwa bodi hiyo aliyoiteua imejaa mabilionea akiwemo Ogunlesi ambaye ndiye Mwafrika pekee.

Ogunlesi aliyezaliwa katika Jimbo la Ondo nchini Nigeria ni mhitimu katika vyuo vya Oxford na Harvard, pia ni Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi wa makammpuni ya Global Infrastructure Partners.

Baba mzazi wa Ogulesi ndiye alikuwa profesa wa kwanza wa udaktari nchini Nigeria.


Wajumbe wengine aliowateua Trump katika bodi hiyo ni pamoja na;

Mwenyekiti wa Bodi, Stephen Schwarzman ambaye ni Mwenyekiti, Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Blackstone.
Paul Atkins, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa General Motors Toby Cosgrove, Mkurugenzi Mtendaji wa Cleveland Clinic Jamie Dimon, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa JPMorgan Chase & Co. Larry Fink, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa BlackRock Bob Iger, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa The Walt Disney Company
Rich Lesser, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Boston Consulting Group Doug McMillon, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Wal-Mart Stores Inc.

Jim McNerney, Mwenyekiti, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Boeing Ginni Rometty, Mwenyekiti, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa IBM Kevin Warsh, Mjumbe wa zamani wa Bodi ya Magavana wa Federal Reserve System Mark Weinberger, Mwenyekiti wa dunia na Mkurugenzi Mtendaji wa EY Jack Welch, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa General Electric
Daniel Yergin, Mshindi wa Tuzo ya Pulitzer na Makamu Mwenyekiti wa IHS Markit

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, kundi hilo litamshauri Trump jinsi ya kuweka mipango itakayochochea ukuaji wa upatikanaji ajira na kuongeza uzalishaji nchini Marekani

No comments :

Post a Comment