Dar es Salaam. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ametakiwa kuishauri Serikali kitaalamu na siyo kisiasa.
Pia, ametakiwa kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kama yanavyoainishwa kwenye sehemu ya pili, kifungu cha nne cha Sheria ya TLS namba 307.
Rai hiyo imetolewa na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha baada ya Dk Mwakyembe kutishia kuifuta TLS kwa madai ya kuingiza siasa kwenye uchaguzi wa viongozi wake mwaka huu.
Awali, Dk Mwakyembe alitoa kauli hiyo alipokutana na sekretarieti ya chama hicho wiki hii na kunukuliwa na vyombo vya habari.
Kutokana na kauli hiyo Masha ambaye ni mmoja wa wagombea urais wa TLS katika uchaguzi utakaofanyika Machi 18, amesema aliposikia kwa mara ya kwanza alishangaa kauli hiyo kutolewa na waziri huyo ambaye amewahi kumfundisha akiwa chuo kikuu.
No comments :
Post a Comment