THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)
THE DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe 27/3/2017
Na. Kurugenzi ya Habari, Uenezi Na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa

TAARIFA MUHIMU ZA WIKI TAREHE 20-26, MACHI, 2017
Hii ni wiki ya saba (7) sasa kukuletea mukhtasari wa taarifa muhimu juu ya masuala mbalimbali kwa lengo la kuwajulisha wanachama, viongozi na watanzania wote kwa ujumla yanayoendelea ndani ya CUF na kuwekana sawia kwa kuwapa “Updates” na aidha kusahihisha taarifa za upotoshwaji, hujuma na au propaganda chafu dhidi ya Chama (CUF Weekly Reports).
KURUGENZI YA HABARI, UENEZI NA MAHUSIANO NA UMMA WIKI HII INAWAJULISHA TAARIFA ZIFUATAZO:-
1. KESI YA WIZI WA FEDHA ZA RUZUKU YA CHAMA-CUF ITAANZA KUSIKILIZWA KESHO TAREHE 28/3/2017 MAHAKAMA KUU: Kesi/Miscellaneous Civil Cause No. 21/2017 ya wizi wa fedha za Ruzuku ya CUF imepangwa kesho tarehe 28/3/2017 Mahakama Kuu mbele ya Mhe.Jaji Dyansobera. WANACHAMA NA WAPENZI WA CUF WOTE MNAOMBWA KUFIKA MAHAKAMANI MAPEMA.
2. MAHAKAMA YATOA AMRI “ORDER” YA KUMZUIA LIPUMBA NA GENGE LAKE KUVAMIA OFISI YA JUMUIYA YA WANAWAKE TAIFA-JUKECUF: Kesi Namba 125/2017 Mahakama ya Ardhi Ilala imetoa amri (Court Order) ya kuzuia uvamizi katika ofisi hiyo iliyopo Vingunguti, Dar es Salaam. Shauri linatajwa kesho tarehe 28/3/2017 kupangiwa tarehe ya kusikilizwa.
3. KUNDI LA MUNGIKI LASHINDWA KUFIKA MAHAKAMANI KUTOKANA NA UKATA WA FEDHA: Kesi namba 23/2016 dhidi ya Msajili Jaji Francis Mutungi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Lipumba na wenzake itatajwa tarehe 10/4/2017. tayari Jaji Kihiyo ameshawapatia mawakili wetu nakala za (ruling, drawn order and proceedings) kwa ajili ya mchakato wa maombi ya Mapitio ya hukumu yake ya kukataa kutoka katika kusikiliza shauri hili (Application for Revision) itakayowasilishwa mbele ya Mahakama ya Rufaa.
Mawakili wetu wameshakamilisha hatua za kisheria za kuomba (Application for extension of time to file Revision) maana muda wa siku 60 wa ku-file Revision Mahakama ya Rufaa umepita kutokana na Jaji Kihiyo kuchelewesha kutoa nakala hizo. Shauri hili liliitwa Mahakama Kuu tarehe 22/3/2017 hata hivyo kundi la Mungiki wote hawakuweza kuhudhuria Mahakamani kutokana na Ukata wa fedha za posho na kukodishia watu mbalimbali na kuweka Mafuta magari mbali na majigambo ya kutaka tukutane mahakamani hapo tarehe hiyo. SHAURI HILI HALITAENDELEA KUSIKILIZWA MBELE YA JAJI KIHIYO MPAKA MAHAKAMA YA RUFAA ITAKAPOTOA MAAMUZI.

4. KESI YA KUWAZUIA SAKAYA NA WENZAKE WALIOSIMAMISHWA NA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA KUFANYAKAZI ZA CHAMA:
Shauri namba 45/2017 (maombi madogo) kutoka kesi ya msingi namba 1/2017 dhidi ya Magdalena Sakaya, na wenzake 7 juu ya kuitisha na kufanya kikao batili cha Kamati ya Utendaji ya Taifa na kufanya kazi zisizowahusu kwa mujibu wa Katiba ya CUF pamoja na kutotambuliwa wala kuthibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa. Imepangwa kusikiliza Tarehe 12/4/2017 katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam. Mbele ya Hakimu Wilbard Mashauri.

5. MKUTANO MKUU WA WILAYA RUANGWA UMEMVUA UONGOZI MWENYEKITI WA WILAYA:
Juzi Tarehe 25/3/2017 wajumbe wa Mkutano Mkuu wa wilaya ya Ruangwa wameazimia kwa kauli moja kumvua uongozi Omary Mohamed LIWIKILA (Mwenyekiti wa Wilaya ya Ruangwa) kwa mujibu wa katiba ya CUF Ibara ya 63(1)(c) na 108(1)(4) kutokana na kufanya vitendo vya kukihujumu Chama na kukiuka maadili na nidhamu ya Chama kwa mujibu wa Katiba. Awali alisimamishwa uongozi na Kamati ya Utendaji ya wilaya. Pamoja nae wengine waliochukuliwa hatua hiyo ni Hamisi Chimale na Bibie Mpilikene waliokuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji wilaya. Katika Mkutano huo ambao ulihudhuriwa na Mhe. Yusuf Salim (MB-Chambani, Pemba) – Naibu Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama CUF-Taifa, Mhe. Abdallah Mtolea(MB-Temeke)- Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa-CUF Taifa, na Mbarala Maharagande- (Naibu Mkurugenzi wa Habari-CUF Taifa) Jeshi la polisi lilizuia kufanyika kwa Mkutano huo katika ukumbi ulioandaliwa rasmi kwa hoja dhaifu kabisa. Wajumbe waliendelea na Mkutano huo katika ofisi ya wilaya ya Ruangwa na kufikia maamuzi hayo.

6. SHEREHE ZA USHINDI WA MITAA 7 LINDI KUFANYIKA TAREHE 8/4/2017:
Tarehe 25/3/2017 iliazimiwa kufanyika kwa sherehe za kuwapongeza wananchi, viongozi na wanachama wa CUF wilaya ya Lindi kwa Ushindi mnono wa heshima walioupatia Chama cha CUF. Sherehe hizo zililazimika kuahirishwa kutokana na misiba ya ndugu wa karibu wa wanaCUF eneo hilo ambalo ulipangwa kufanyika Mkutano wa Hadhara, Kikao cha Ndani na Kutoa Tuzo ya Nishani maalum kwa wapambanaji wote. Viongozi walitajwa hapo juu waliokwenda wilayani Ruangwa walifanya kikao kidogo cha ndani na viongozi wa Lindi na kuwapongeza kwa msimamo thabiti wa kukisimamia Chama.

7. OCT- WILAYA YA TEMEKE INAENDELEA VYEMA: vikao vya OCT wilaya ya Temeke vinaendelea vyema na tayari washtakiwa watatu (Mungiki) akiwemo Sawaka Sawaka, na Kindeku, waliofanya uvamizi na kuwashambulia wanachama wakiwa katika kikao cha OCT na kuwaumiza baadhi ya wanachama pamoja na Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyambwela Musa Bakari wamekamatwa na kufikishwa kituo cha Polisi, Changombe. Upelelezi unaendelea kwa kufungiliwa kesi ya Jinai.
8. MKURUGENZI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MHE. ISMAIL JUSA AENDELEA NA ZIARA NJE YA NCHI:
Kwa wiki ya nne sasa Mhe. Ismail JUSA anaendelea na ziara maalumu ya kushughulikia masuala mbalimbali ya CUF kimataifa. Baada ya kukamilisha ziara hiyo nchini Marekani, hivi sasa anaendelea na ziara hiyo nchini Uingereza. Amepata fursa ya kukutana na viongozi mbalimbali wa kisiasa. Ametuma salamu na kutaka tuwajulishe kuwa MAMBO YETU NA JAMBO LETU LIMEKAA VIZURI SANA. TEMBEENI KIFUA MBELE HAKI TAYARI IPO MIKONONI.

9. MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI TAIFA MHE. JULIUS MTATIRO AMEKIWAKILISHA CHAMA KATIKA MKUTANO MKUU WA VYAMA VYA KILIBERALI (AFRICAN LIBERAL NETWORK-ALN) ULIOFANYIKA TAREHE 23-26/3/2017 NAIROBI, KENYA. Mkutano huo ulitanguliwa na Mkutano wa Vijana wa kiliberali ambapo CUF iliwakilishwa na Hamisi Kapalila ambae ni Mratibu wa Afrika Mashariki (African Liberal Network-Youth Coordinator in East africa) Aidha, pia Jumuiya ya vijana Taifa-JUVICUF imetuma wawakilishi wanne nchini UGANDA, kuhudhuria Mafunzo ya Uongozi na Siasa kwa vijana chini ya PROGRAMME FOR YOUNG POLITICIANS IN AFRICA-PYPA; Mwl. Razaq Mtele Malilo, Rachel Nyarusanda Bugingo, Mohamed Ibrahim Rajab (Mohabeshy)(ZNZ) na Makkiye Juma Ali (ZNZ), wamekiwakilisha Chama.
HII NDIO CUF TAASISI IMARA NA YENYE VIONGOZI MAKINI INAVYOFANYA KAZI ZAKE. INATAMBULIKA KITAIFA NA KIMATAIFA KWA UIMARA WAKE. VIBARAKA WALIOJIPAKAZI YA KUTAKA KUKIYUMBISHA CHAMA TUTAPAMBANA NAO KWA MIKAKATI THABITI YA KIAKILI NA MAARIFA MAKUBWA NA KAMWE HAWATAFANIKIWA.
8. BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA LIMEFANYA KIKAO CHAKE CHA KAWAIDA MJINI UNGUJA, ZANZIBAR NA KUAZIMIA MASUALA MUHIMU KWA USTAWI WA CHAMA: Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) lilikutana Jumapili ya tarehe 19 Machi, 2017 katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama iliyopo Vuga, Mjini Unguja-Zanzibar. Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wajumbe halali 43 kati ya wajumbe wote Halali 53 na Wajumbe wanne (4) kati ya hao hawakuweza kuhudhuria kwa kutoa udhuru kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuwa nje ya nchi. Wajumbe hao ni Ismail Jussa, Ahmed Marshed, Juma Mkumbi, Hashimu Mziray na Mama Kimey ambae ni mgonjwa wa muda mrefu(Mwenyezi Mungu Amponye kwa Baraka zake). Pamoja na Maazimio mengine;
– Baraza Kuu limepokea taarifa rasmi za uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki wanaopaswa kudhaminiwa na Chama ikiwemo ratiba ya uchaguzi huo na taratibu zake kutoka ofisi ya Katibu wa Bunge – Dodoma. Baraza Kuu kwa mujibu wa Katiba ya Chama Ibara ya 104(1) imemteua; *Mheshimiwa Twaha Issa Taslimu* kuwa Mgombea wa Chama cha CUF kwa nafasi hiyo. Mheshimiwa Twaha pia ndiye Mbunge anayetokana na CUF wa bunge hilo la Afrika Mashariki anayemaliza muda wake kwa sasa.
– Baraza Kuu limepokea taarifa na kubariki hatua hizo za kuvuliwa uanachama kwa wanachama wafuatao: Mohamed Habibu Mnyaa- Tawi la Mkanyageni jimbo la Mkoani-Pemba, Haroub Shamis- Tawi la Kipepo jimbo la ChakeChake –Pemba, Mussa Haji Kombo- tawi la Miembeni Jimbo la Chakechake –Pemba, Khalifa Suleiman Khalifa- tawi la Junguni Jimbo la Gando-Pemba, Thiney Juma Mohamed – tawi la Kidato Jimbo la Mtopepo-Unguja, Nassor Seif Amour- Tawi la Kangani Jimbo la Mtambile-Pemba, Rukia Kassim Ahmed- Tawi la Wawi Jimbo la Wawi-Pemba. Hawa wote kwa sasa si wanachama wa CUF.
– Baraza Kuu limepitisha Programu Ya Kuimarisha Chama nchini itakayoratibiwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa. Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma Mhe. SALIM BIMAN anawajulisha wananchi wote wa kisiwa cha Unguja kuwa Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad ataanza ziara ya Uimarishaji Chama katika wilaya zote saba (7) kisiwani Unguja, ziara inafuatiwa baada ya ziara iliyopata mafanikio Makubwa ya Kisiwani, Pemba. Ziara hiyo itaambatana na ufunguaji wa ofisi mpya za Chama, kuweka waratibu wa Chama, kufungua matawi mapya, na kuwasikiliza wananchi na kutoa muelekeo na misimamo ya CUF kwa kipindi hichi. Baada ya kukamilisha Unguja Ziara hizo zitaanza kwa wilaya mbalimbali za Tanzania Bara.
– Na Kuteua Bodi Mpya ya WADHAMINI WA CHAMA CHA CUF ili kukidhi haja na matakwa ya Katiba Mpya ya CUF ya mwaka 2014. Uteuzi huu haubatilishi bodi iliyokuwepo awali na taarifa zake tumeziambatanisha na waraka huu.

9. MUELEKEO WA TAASISI YA CUF (THE WAY FORWARD)
Kutokana na Uchaguzi wa ndani ya Chama uliofanyika June 28, mwaka 2014 Mkutano Mkuu wa Taifa uliwachagua viongozi mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Baraza Kuu ukijumuisha na wale wanaoingia kwa nafasi zao Jumla ya Wajumbe ni 63 tu. Wapo wajumbe waliofariki (1), kuhama Chama (2), kusimamishwa (5) na kufukuzwa (2). Kutokana na mahudhurio ya wajumbe 43+5=48 katika kikao cha Zanzibar tarehe 19/3/2017 wajumbe halali wasiohudhuria kikao hicho ni 5 na hata ukijumlisha waliosimamishwa 5 jumla ni wajumbe 10. Hakuna Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la wajumbe 10. Lipumba anaelekea kufilisika kisiasa. Alikuwa akimsema JK kuwa ni msanii wa kisiasa naona sasa nafasi hiyo ameirithi yeye. Kinachoendelea Buguruni Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Chama Taifa ni Mazingaombwe ya kisiasa. Wanachama, Viongozi, wapenzi wa CUF na wanaopenda mabadiliko wote nchini ONDOENI KHOFU. Viongozi wenu CUF Taifa tumejipanga NGANGARI kukabiliana na upuuzi huu wa KI-INTARAHAMWE anaoufanya Lipumba na genge lake. Hatua mbalimbali zinaendelea kufanyiwa kazi. Lipumba hana uhalali wa kikatiba (Constitutional Legitimacy) kufanya anachofanya. Kamwe wanachama wa CCM, ADC, CHAUSTA, ACT na wale waliofukuzwa na kuvuliwa uanachama wa CUF waliohudhuria kikao cha ‘kigodoro’ Buguruni hawawezi kuwa WAJUMBE WA BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA. BARAZA HARAMU NA MAAMUZI YAKE YOTE NI HARAMU. Tutafanya uchambuzi mpana wa haya yanayoendelea sasa mbele ya waandishi wa habari siku chache zijazo. CUF ina Baraza Kuu Moja, Kamati ya Utendaji Moja, na Bodi ya wadhamini Moja. Inayosimamiwa na Katibu Mkuu wa Chama Maalim Seif Sharif Hamad, na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa Mheshimiwa Julius Mtatiro. Endelee kutekeleza majukumu yenu katika maeneo yenu na kuwashughulikia wale wote wanaoonekana kwenda kinyume na Katiba ya Chama. Hakika Haki itakuwa juu ya Upotofu.

HAKI SAWA KWA WOTE
———————————————-
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA- CUF TAIFA
MAWASILIANO: 0784 001 408/0715 062 577
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA- CUF TAIFA
MAWASILIANO: 0784 001 408/0715 062 577
No comments :
Post a Comment