Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 26, 2017

JWTZ yadaiwa na Tanesco Sh3bilioni!


Dar es Salaam. Mkuu wa Majeshi nchini, Evance Mabeyo amesema Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) linadaiwa Sh3 bilioni na Shirika la Umeme nchini na kesho (Jumatatu) watapunguza deni hilo ili wasikatiwe umeme.

Mabeyo ameyasema hayo leo wakati anazungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi (Ngome) na kueleza deni hilo limetokana na shughuli za jeshi hilo kwenye ulinzi wa Taifa pamoja na ufinyu wa bajeti.

"Baada ya kupokea maelezo ya Tanesco na kufuatia tamko la Rais, Jeshi la Wananchi limetafakari na limefanya jitihada kupata fedha za kupunguza deni hili, tunadaiwa fedha kiasi kinachozidi kidogo Sh3 bilioni, nimeagiza watendaji wetu watafute Sh1 bilioni," amesema Mabeyo.

Mabeyo amesema juhudi zinazofanywa na Jeshi hilo zinatakiwa kuonyeshwa na Taasisi nyingine ili kuweza kuiongezea Tanesco uwezo wa kutoa huduma.



No comments :

Post a Comment