Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, March 28, 2017

Serikali yakiri kukwama kupata mkopo wa nje!

Serikali imeshindwa kupata fedha za mkopo wa nje yenye masharti ya kibiashara katika bajeti ya mwaka 2016/17 kutokana na hali ya soko la fedha la kimataifa kutokuwa nzuri hasa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka huo wa fedha.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hayo bungeni wakati akiwasilisha mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ya kiwango na ukomo wa bajeti ya Serikali.

Amesema kuwa katika mwaka huo wa fedha Serikali ilipanga kukopa katika vyanzo vya kibiashara Sh2100.9 bilioni ili kugharamia miradi ya maendeleo nchini.

“Katika kipindi hicho riba ilipanda kutoka wastani wa asilimia sita hadi asilimia tisa. Kutokana na sababu hiyo Serikali iliahirisha mchakato wa kukopa kutoka kwenye masoko hayo,”amesema.

Hata hivyo, amesema gharama ya ukopaji katika masoko ya ulaya imeanza kuimarika.

No comments :

Post a Comment