dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, June 20, 2017

Magufuli aishushia Neema Pwani, Alia na Mafisadi!


Pwani. Rais John Magufuli amewatangazia neema wakazi wa mkoa wa Pwani baada ya kuwaahidi kuwa itajengwa bandari kavu eneo la Ruvu, ambayo mizigo inayotoka nchi jirani itapitishwa katika bandari hiyo.

Ameyasema hayo leo (Jumanne) wakati akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kwanza na wananchi wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoa wa Pwani.

“Ni fursa kubwa kwa wakazi wa Ruvu, Pwani, tunafanya hivi kwa niaba yenu,” amesema.

Amesema pia itajengwa barabara ya kisasa Dar Express way, itakayotoka Dar es Salaam, kwenda Chalinze ambayo itakuwa na njia sita pamoja na barabara za juu.

“Tanzania ni tajiri, lazima tuwe na maisha ya kitajiri badala ya kuwa matajiri na kuwasindikiza wenzetu katika utajiri,” amesema.

No comments :

Post a Comment