dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, July 17, 2017

Wananchi na Viongozi nusura wazichape Babati!

Mvutano mkali umeibuka katika mkutano wa hadhara wa kisheria baina ya wananchi kata ya Galapo kijiji cha Hallu wilaya ya Babati na viongozi wa serikali ya kijiji hicho huku wananchi wakionyesha kukosa imani na uongozi kutokana na udanganyifu uliofanywa na wajumbe wa serikali ya kijiji katika ugawaji wa ardhi kwaajili ya mashamba kwa vijana ambapo wajumbe wa serikali ya kijiji walijigawia jumla ya hekari 62.
Ni mtifuano baina ya wananchi na viongozi wao unaopelekewa na mgogoro wa ardhi uliodumu tangu mwaka 2012 ambapo wananchi wanadai viongozi kufanya udanganyifu katika upimaji wa eneo la ardhi lililopo eneo la nyamwali baada ya maamuzi ya mkutano mkuu wa kijiji kuamua kupimwa maeneo hayo na kugawiwa jumla ya vijana 240 lakini hali ikawa ni tofauti kutokana na eneo kuhakikiwa mara mbili na kuonyesha ukubwa ulio kinzana hivyo kuwaacha wananchi katika maswali na hisia tofauti.

Hata hivyo Katibu tarafa babati alijaribu kutuliza hasira za wananchi hawa kwa niaba ya mkuu wa wilaya kwa kuundwa tume kwaajili ya kuhakiki kwa mara nyingine tume ambayo itaongozwa na wananchi wenyewe.

Lakini Simon Laway ni mwenyekiti wa kijiji hiki ambaye yeye alibebeshwa lawama zaidi.

Hata hivyo wananchi hao wameiomba serikali ngazi ya wialaya hatimaye mkoa kuingilia kati mara moja mgogoro huu ili kuzuia kuendelea kuwa mkubwa zaidi.

No comments :

Post a Comment