dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 4, 2017

Fahamu jinsi ya kukadiria kiasi cha kodi unachotakiwa kulipa TRA kabla ya kuagiza gari kutoka nje ya nchi!

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA sasa imesogeza huduma karubu zaidi na wateja kwa kutengeneza kurasa ya kielectroniki itakayo msaidia mteja kujua gharama ya kodi kwa Gari anayo agiza kulingana na hali ya gari husika.

Kurasa hizo zimekuwa zikitumiwa na mamia ya watu katika kupanga bajeti zao binafsi kabla ya kuamua kufanya manunuzi ya bidhaa hasa magari nje ya nchi.

Ili kuweza kukokotoa kiasi halisi cha kodi ambacho TRA wanaweza kukukata kabla ya kumua kuagiza gari ililotumika kutoka nje ya nchi, tembelea tovuti ya TRA kipingere cha Quick Links na hapo chagua Calculators & Tools au unaweza ukabonyeza hapa.Utaletewa fomu ya kujaza taarifa za gari unaotaka kuagiza kama aina ya gari, kampuni iliyotengeneza, aina ya bodi, mwaka wa iliotengenezwa na nchi unapotaka kuiagiza, uwezo wa injini na mafuta.

Hapa kitu cha muhimu zaidi kukifahamu ni mwaka ambao gari limetengenezwa na uwezo wa injini (Engine Capacity (cc)). Kodi huongezeka zaidi kulingana na mwaka ambao gari limetengenezwa, gari linapozidi kuwa la zamani na kiasi cha kodi huongezeka maradufu, hii ni kuendana na sera za nchi yetu na sera za kimazingira ili kupunguza idadi ya magari mabovu yanayoagizwa nchini.


Baada ya kujaza taarifa zote za muhimu za gari unalotaka kuagiza au uliloagiza bonyeza ‘Calculate Taxes’ na hapo utaletewa kiasi cha kodi unachotakiwa kulipa.

No comments :

Post a Comment