Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Friday, August 4, 2017

Mwanamume aliyeingizwa kwenye jeneza Afrika Kusini atoa ushahidi Mahakamani!

Mwanamume mmoja mweusi ambaye anadaiwa kulazimishwa kuingia ndani ya jeneza na wanaume wawili wazungu ambao walitisha kumchoma akiwa hai ametoa ushahidi mbele ya mahakama nchini Afrika Kusini.

Victor Mlotshwa alingua kilio kwenye mahakama kuu ya Middleburg wakati alikumbuka kisa hicho cha mwezi Agosti mwaka uliopita.

Mahakama ilicheza video ya kisa hicho ambapo bwana Mlotshwa anaweza kusokika akilia na kuomba washambuliaji kumsamehe.Anadai kuwa wakulima Theo Jackson na Willem Oosthuizen walimfunga kwa nyaya wakampiga na kutishia kumpiga risasi.

Washukiwa hao wawili wanakana hilo wakidai kuwa walimpata bwana Mlotswa akiiba nyaya.

Wanasema kuwa lengi lao lilikuwa ni la kumfunza adabu. Kisa hicho kilizua ghadhabu kubwa nchini Afrika Kusini.

No comments :

Post a Comment