Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Wednesday, August 2, 2017

HEALTH: Faida za kula Choroko kiafya!

Je wewe ni miongoni mwa wapenzi wa choroko? Kama unatumia utakuwa miongoni mwa wanaofaidika na virutubisho muhimu kwa afya mwilini.

Wataalamu waliofanya uchunguzi kuhusu choroko ambayo ni jamii ya kunde,
wanasema utamu wa ladha yake unashabihiana kabisa na umuhimu wake katika afya.

Zifuatazo ndizo faida za kula choroko;
Choroko ni kati ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha protini, madini ya phosphorus na calcium. Ukiachilia mbali faida nyingine, virutubisho hivi ni muhimu sana kwa ustawi wa afya ya ubongo.Wataalam mbalimbali wamenukuliwa na mtandao wa kesehatan.123.com wakielezea umuhimu wa ulaji wa choroko ili kuongeza uwezo wa kufikiri.

Faida nyingine za choroko ni pamoja na kuimarisha mifupa. Hii inatokana na kiwango kikubwa cha madini ya phosphorus na calcium.

 Choroko pia ni nzuri kwa afya ya moyo, mafuta yaliyopo kwenye mboga hii ni salama na yana faida katika kuusaidiana moyo kutenda kazi zake vizuri na kwa upande mwingine kusaidia kurahisisha ufyonzwaji wa chakula mwilini* hivyo kuepuka hatari ya kupata saratani.

 Uwepo wa vitamin B1 na B2* ndani yake husaidia kuimarisha mfumo wa fahamu nasi vizuri kutumiwa na wajawazito kwa sababu zina kiwango kikubwa cha folic acid ambayo ni muhimu kw aukuaji wa mtoto.

No comments :

Post a Comment