dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 2, 2017

Mwizi apatikana amelewa ndani ya nyumba aliovunja!

Mtu mmoja ameshtakiwa na maafisa wa polisi nchini Australia baada ya kuvunja na kuingia katika nyumba moja kabla ya kunywa shampeni na kulala kitandani.

Polisi wanasema jamaa huyo wa miaka 36 alivunja na kuingia nyumbani humo mjini Esperence, magharibi mwa Australia siku ya Ijumaa.

Alilewa baada ya kunywa kinywaji hicho ,kulingana na maafisa, Mwenye nyumba hiyo alirudi nyumbani na kumpata mwizi huyo amelala kitandani mwake.

''Alitoka nje na kuwapigia simu polisi ambao waliwasili na kumkamata mshtakiwa'', alisema sajenti Richard Moore kutoka polisi ya Esperence, Mtu huyo alipelekwa hospitalini baada ya kupatikana amelewa chakari alisema sajenti Moore.

No comments :

Post a Comment