dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 10, 2017

HEALTH: Aina saba za vyakula vimfaavyo mgonjwa wa kisukari!

Chakula bora kabisa kwa mgonjwa wa kisukari ni kile ambacho ni chakula cha asili na si kile ambacho kimetengenezwa kiwandani.Unahitaji chakula ambacho hakijakobolewa, unahitaji zaidi matunda na mboga za majani. Kutumia vyakula hivi naenda kukueleza kwenye hii makala kutakusaidia kupata mahitaji ya viinilishe unavyohitaji wakati huo huo ukipunguza matatizo yanayoweza kuletwa na kisukari ikiwemo hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo.

Ndiyo, si vyakula hivi tu kwenye hii orodha ndivyo unavyopaswa kuwa unakula, bali kuvijumuisha vyakula hivi kwenye mlo wako kila siku kutakusaidia kuimarika kwa afya yako kwa ujumla.

Kama tayari unafuata mlo wenye afya wenye matunda, mboga za majani na kula vyakula ambavyo havijakobolewa naomba nikupe hongera mapema. Upo njiani kuelekea kwenye maisha ya afya bora na marefu na unaelekea kwenye hatua za kudhibiti uzito wako na kiasi cha sukari kwenye damu yako.

Vyakula hivi naenda kuvijadili siyo tu vina nyuzinyuzi za kutosha, madini, vitamini na viuavijasumu tu, lakini pia vyakula hivi vinapatikana kirahisi kwenye mazingira yetu na vinapatikana kwa bei rahisi.

Kula ugali wa dona na uachane na ugali wa sembe, kama ni mkate tumia mkate wa ngano ambayo haijakobolewa (brown bread), kunywa maji mengi bila kusahau kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku.

Kisukari ni ugonjwa wa tabia, ni matokeo ya kile unachokula na kunywa kila siku.
Wapo watu hawaamini kama unaweza kupona Kisukari lakini kama utaamua kula chakula sahihi kwa muda mrefu, ukawa bize na mazoezi kila siku, ukinywa maji ya kutosha kila siku na kutumia chumvi ya kutosha kwenye vyakula vyako kila siku kupona inakuwa ni jambo la kawaida.

Chakula cha mgonjwa wa kisukari aina ya pili

1. Parachichi
Parachichi linajulikana kwa kuwa na mafuta mazuri kwa ajili ya moyo (monounsaturated fat).
Mafuta ya namna hii kama yanayopatikana kwenye tunda la parachichi yanaweza kuweka sawa usawa wa kolesto mwilini, yanaweza kupunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo na hivyo kuwa tunda zuri kwa mtu mwenye kisukari.

Parachichi ni tunda zuri sana kwa mtu anayesumbuliwa na kisukari aina ya pili.
Parachichi ni tunda ambalo sababu ya mafuta yake mazuri, sababu parachihchi moja laweza kuwa na mpaka gramu 16 za mafuta linatakiwa lichukuliwe kama mafuta.

Wakati huo huo parachichi moja lina nyuzinyuzi gramu 2 na wanga gramu 2.
Unaweza kula parachichi lenyewe kama lilivyo, unaweza kuongeza kwenye kachumbali mbalimbali au ukanywa juisi yake kila siku.

2.  Maharage
Maharage ni moja ya matunda au mboga za ajabu sana watu wengi hawajuwi.
Kile nataka nikujulishe kupitia makala hii ni kuwa maharage yana nyuzinyuzi (faiba) ya kutosha kwa mahitaji yako ya kila siku na si hivyo tu maharage yana protini bora kabisa kuliko zote isiyo na madhara kama ile ya kwenye wanyama na hizi ndizo sababu maharage ni chakula kizuri sana kwa mtu mwenye kisukari na mwenye shinikizo la juu la damu pia.

Vile vile kutumia vyakula vyenye nyuzinyuzi zaidi kunakuondolea hatari ya kupatwa na mishtuko ya moyo (stroke).
Inasisitizwa upate walau gramu 25 za faiba kila siku. Kikombe kimoja cha maharage yaliyopikwa kina mpaka gramu 9 za faiba.

Inashauriwa kwa watu wenye kisukari kula gramu 25 mpaka 30 za maharage machanga ya kijani kibichi au njegere (green beans), siagi halisi na chumvi dakika 15 kabla ya kwenda kulala, hii itasaidia kushusha damu sukari waamkapo asubuhi.

Maharage haya yana kiasi kidogo cha wanga (carbs), na kiasi kingi cha protini, magnesiamu na asidi amino iitwayo ‘tryptophan’ ili kuubeba mwili usiku mzima.
Jaribu kutumia maharage kama chanzo kikuu cha protini kila siku na vizuri zaidi ni kuwa yanapatikana kwa bei rahisi zaidi ukilinganisha na nyama au samaki.

3.  Samaki
Samaki ni chakula bora kwa mgonjwa wa kisukari. Samaki wana omega 3 ambayo ni nzuri kwa mtu anayetaka kuepuka kolesto na kisukari kwa ujumla.
Omega 3 pia ni nzuri kwa mtu mwenye presha ya kupanda na hupunguza uwezekano wa kutokea tatizo la kupoteza kumbukumbu na ukichaa.

Pamoja na hayo nakushauri utumie samaki wa hapa hapa kwetu Tanzania na siyo wale kutoka nje kwani wengine wanavuliwa kwa namna ambayo si salama kwa afya. Kula samaki kila mara kama unasumbuliwa na kisukari.

4. Kitunguu swaumu
Kitunguu swaumu ni kiungo kizuri kwa chakula sababu ya harufu yake nzuri ya kupendeza na wakati huo huo ni dawa nzuri sana kwa magonjwa mbalimbali mwilini ikiwemo kisukari.

Kitunguu swaumu kwa miaka mingi kimetumika kutibu kolesto, magonjwa ya moyo, shinikizo la juu la damu na kansa. Hizi ndizo sababu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa chakula bora kwa mtu mwenye kisukari.

Hata hivyo ili kitunguu swaumu kiwe kizuri kama tiba ni vizuri kitumike kibichi yaani bila kupikwa katika moto.
Katakata punje 3 za kitunguu swaumu na unywe na maji vikombe viwili kama unavyokunywa dawa nyingine za kawaida kila unapoenda kulala.
Ukishakuwa umevikatakata inashauriwa uviache kwanza katika hewa kwa dakika 10 ndipo umeze kwa matokeo mazuri zaidi.

5. Tikiti maji
Ukipata hamu ya kutaka kula au kunywa chochote kitamu hasa hivi vya dukani basi wewe kimbilia kula tikiti maji au hata juisi yake.

Kama ilivyo kwa nyanya, tikiti maji pia lina viuavijasumu mhimu sana (lycopene) ambavyo vinaweza kusaidia kukukinga dhidi ya baadhi ya kansa na kudhurika kwa seli kunakohusiana na magonjwa ya moyo.
Tikiti maji pia ni zuri pia kwa mtu mwenye kolesto.

6. Tufaa (Apple)
Kuna msemo wa kizungu unasema: ‘An apple a day keeps the doctor away’, inamaanisha kula tunda moja la tufaa kwa siku kunaondoa uhitaji wa daktari hasa daktari wa matatizo ya moyo.
Kula tufaa moja tu kwa siku kwa wiki 4 kunaweza kupunguza kolesto mbaya mpaka asilimia 40. Kuna aina ya viondoa sumu vilivyomo kwenye tufaa ambavyo huwezi kuvipata sehemu nyingine yoyote na ndiyo vinalifanya tunda hili kuwa tunda mhimu zaidi kutumika na mtu mwenye kisukari kila siku.

Tunda hili tamu limeonekana kutoa ulinzi mkubwa kwa watu wenye kisukari hasa kisukari aina ya pili. Tufaa moja dogo la kawaida lina gramu 3 za nyuzinyuzi (fiber), nyuzinyuzi ni kitu kingine mhimu kwa mgonjwa wa kisukari.
Kumbuka pia lakini tufaa moja lina wanga gramu 15 hivyo usile zaidi ya moja kwa siku.

7. Karoti
Zilizopikwa au zikiwa freshi ni mboga nzuri kuongezwa kwenye chakula chochote. Karoti zina kiasi kingi cha vitamini A, viuavijasumu mhimu zaidi ‘beta-carotene’.
Vitamini A ni mhimu sana kwa matatizo ya macho, kuzuia kansa na kinga ya mwili vitu viwili mhimu sana kwa mtu anayesumbuliwa na Kisukari.
Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali hii beta-carotene inao uwezo wa kuzuia usipatwe pia na kisukari hasa kisukari aina ya pili.
Pendelea kutafuna karoti mbichi zaidi na siyo zilizopikwa kwa matokeo mazuri.

No comments :

Post a Comment