dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 14, 2017

Kinana: Siyo dhambi wala kosa chama cha upinzani kushinda!


Nzega. Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahman Kinana amesema siyo nongwa vyama vya upinzani kushinda uchaguzi.
Akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Nzega vijijini jana Jumatano, Kinana alisema vyama vinapoingia kwenye mchakato wa uchaguzi, kila kimoja kina haki ya kushinda kulingana na sera, mikakati, uungwaji mkono na kukubalika kwa wapiga kura, hivyo ni sawa hata pale mshindi anapotoka chama cha upinzani iwapo ndiyo maamuzi ya wapiga kura.

“Siyo dhambi wala kosa chama cha upinzani kushinda kata au jimbo; ni sawa tu kwa sababu sote tunakuwa kwenye uchaguzi kushindanisha sera. Kwanza hao wapinzani ni watani na marafiki zetu kisiasa,” alisema Kinana

Kauli hiyo ya Kinana inakuja katika kipindi ambacho kuna dalili za baadhi ya viongozi wa Serikali na chama hicho tawala katika ngazi mbalimbali nchini kuchukulia kuwa ni kosa vyama vya upinzani kushinda uchaguzi katika maeneo yao.

Awali, taarifa ya Katibu wa CCM mkoa wa Tabora, Janeth Kayanda aliyoitoa kwa Kinana ilieleza kuwa chama hicho kilishinda kata 45 kati 46 za wilaya ya Nzega yenye majimbo matatu ya uchaguzi ya Bukene, Nzega mjini na Nzega vijijini.

Katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, kata moja ya Bukene ilinyakuliwa na mgombea kupitia tiketi ya Chadema.

“Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, CCM tulishinda kata 45 katika wilaya ya Nzega yenye majimbo matatu ya Bukene, Nzega mjini na Nzega Vijijini; upinzani ulishinda kata moja,” alisema Kayanda.


/ Mwananchi:

No comments :

Post a Comment