Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa wito kuwa, Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma liwe linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua mali, madeni na maslahi ya viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.
Zitto amewasilisha Muswada Binafsi wa Sheria ili kuweka vifungu vitakavyolazimisha Bunge kuweka wazi muhtasari wa matamko ya Mali na Madeni ya Wabunge (wakiwemo Waziri Mkuu na Mawaziri).
No comments :
Post a Comment