Rais John Magufuli amesema kiwango cha mizigo inayokwenda nchini Rwanda kupitia bandari ya Dar es Salaama kimeongezeka mpaka kufikia tani 95,000 kwa mwaka jana licha ya biashara baina ya nchi hizi mbili kupanda na kushuka.Amesema amekubaliana na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ambaye amefanya ziara ya siku nchini leo na kuondoka saa tisa alasiri kuhakikisha wanahamasisha wafanyabiashara wa nchi zao kujenga mazingira mazuri ya biashara.
Akizungumza na vyombo vya habari Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alisema kumekuwepo na vipindi vya kupanda na kushuka kwa biashara baina ya mataifa haya mawili lakini Serikali zote mbili zimejipanga kujenga mazingira wezeshi ya kibiashara ikiwemo kujenga reli ya kisasa kutoka Isaka (Tanzania) hadi Rwanda.
Amebainisha kwamba mwaka 2011 biashara kati ya Tanzania na Rwanda ilikuwa na thamani ya Sh Bilioni 106.5 mwaka 2012 ilishuka hadi bilioni 27.3, mwaka 2013 ilikuwa Sh 132.2 bilioni, mwaka 2014 Sh 64.45 bilioni na mwaka 2015 ilikuwa Sh 83.95 bilioni.
" Sasa unaweza kuona trend, biashara inapanda na kushuka, sasa kwenye mazungumzo yetu tumekubaliana biashara kati ya nchi zetu mbili ianze kupanda kwa kasi," alisema Rais Magufuli.

No comments :
Post a Comment