Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 15, 2018

KENYA: Akamatwa kwa kumchoma moto baba yake!

Jeshi la Polisi huko Bomet nchini Kenya, linamshikilia kijana mmoja kwa tuhuma za kumchoma moto baba yake mzazi.Polisi wa eneo hilo wamesema mzee huyo alikwenda kwenye duka la familia ambako mtoto wake huyo yupo na kula vitafunwa, na alipotoka kijana wake alimfuata na kumwagia mafuta ambayo yanaaminiwa ni petroli na kumuwasha moto.

“Baba mtu alipoenda kupata vitafunwa, mmiliki wa duka alimfuata na kumwagia mafuta ambayo tunaamini ni petroli na kumchoma moto”, amesema mkuu wa polisi wa eneo hilo la Bomet, Samson Rukunga.

Mzee huyo aliyechomwa moto amekimbizwa kwenye hospitali ya misheni ya Tenwek ambako anapatiwa matibabu, kutokana na kupata majeraha makubwa ya moto.

No comments :

Post a Comment