Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 16, 2018

Mugabe amuunga mkono kiongozi wa upinzani Zimbabwe!


Chama cha National Patriotic Front, NPF, kilichoundwa na waliokuwa mawaziri wa Zanu PF kimemtangaza Rais wake.
Chama hicho kipya kimetangaza kuwa Brigedia mstaafu Ambrose Mutinhiri atakuwa Rais wake, hatua ambayo inaelezwa kuungwa mkono na Robert Mugabe.

Ijumaa ya juma lililopita, Mutinhiri alijiuzulu ubunge na ndani ya Zanu PF, akionyesha kutounga mkono kuondolewa kwa Mugabe madarakani.

Mkutano wa Mugabe wa kwanza na waandishi wa habari tangu aondoke madarakani inasemekana uliandaliwa na chama cha NPF ambacho kina matumaini ya kumuondoa Mnangagwa kwenye kinyang'anyiro cha mwezi Agosti.

Kwa miezi kadhaa sasa imekuwa ikidhaniwa kuwa huenda Mugabe atarejea tena kwenye ulingo wa siasa dhidi ya chama chake cha zamani.

No comments :

Post a Comment