Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, April 2, 2018

Mtolea: "Hakuna siasa Tanzania"!

Mbunge wa Temeke (CUF), Mh. Abdallah Mtolea  ameweka wazi kwamba kwa sasa hakuna siasa zinazofanyika nchini Tanzania kwani vyama vingine vyote vimefungwa isipokuwa Chama Cha Mapinduzi ndicho kinachoonekana kufanya shughuli hizo.
Katika mahojiano na ww.eatv.tv, Mtolea amesema siasa zinafanywa za upande mmoja huku wengine wakiwa wamefungwa na kuongeza kuwa ni kama wameingizwa ulingoni wakiwa wamefungwa mikono huku wanayepigana naye akiwa ameachiwa kuwapiga jinsi anavyotaka.

Aidha Mbunge huyo ameongeza kwamba amesikia kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Ndg Humphrey Polepole anafanya ziara ya nchi nzima kufanya shughuli za kisiasa lakini vyama vingine wamefungwa.

Pamoja na hayo Mbunge Mtolea amesema kwamba vyama vya upinzani vinakosa  sehemu ya kujipambanua hali ambayo inawafanya wazidiwe kwani kwa upande wa CCM baadhi ya viongozi wa Serikali wamekuwa wakifanya kazi za kichama katika majukwaa yao hali ambayo ameiita haina usawa katika uwanja wa siasa.

No comments :

Post a Comment