dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 3, 2018

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA KITUO CHA RADA, APOKEA NDEGE YA TATU YA BOMBADIER!

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wengine akifunua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa mfumo wa rada za kuongozea ndege za kiraia katika vituo vinne vya JNIA, KIA, Mwanza na Songwe iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa kimataiafa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  Aprili 2, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipata maelezo ya toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa anga TCAA Bw. Hamza Johari katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa mfumo wa rada za kuongozea ndege za kiraia katika vituo vinne vya JNIA, KIA, Mwanza na Songwe iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa kimataiafa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 2, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu kama Diamond ambaye alikuwepo kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi la uzinduzi wa mradi wa mfumo wa rada za kuongozea ndege za kiraia katika vituo vinne vya JNIA, KIA, Mwanza na Songwe iliyofanyika kwenye uwanja wa ndege wa kimataiafa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 2, 2018.
Ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 ikipigiwa saluti ya maji baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, na kupokelewa na umati mkubwa wa wananchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Aprili 2, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na viongozi wa dini na wa ATC ndani ya ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, Aprili 2, 2018.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitelemka kutoka kwenye ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 ilipoipokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, Aprili 2, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Zoka huku akishuhudiwa na marubani mara baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, Aprili 2, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akishangiliwa na umati wa wananchi baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, Aprili 2, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipongezwa na Mwenyekiti wa Tanzania society of Travel Agents (TASOTA) Bw. Mustafa Khataw baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, Aprili 2, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipongezwa na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani ya KKKT Dkt. Alex Malasusa baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, Aprili 2, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiaga baada ya kupokea ndege ya tatu ya Bombadier 8 Dash Q-400 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Montreal, Canada, Aprili 2, 2018. 

Picha na IKULU

No comments :

Post a Comment