Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, May 12, 2018

Ufaransa yaigomea Marekani kuhusu Iran!

Ufaransa imesema kuwa haitokubali hatua ya Marekani kuziwekea vikwazo kampuni zinazofanya biashara na Iran.

Kitendo hicho cha Washington kinajiri kufuatia hatua ya rais Donald Trump kujiondoa katika makubaliano ya kihistoria ya kusitisha mpango wa kinyuklia wa Iran.Waziri wa maswala ya kigeni nchini Ufaransa Jean-Yves Le Drian alisema kuwa kampuni za Ulaya hazifai kuathirika kutokana na uamuzi wa Marekani.

Marekani inasema kuwa kampuni zina miezi sita kusitisha biashara na hazitaruhusiwa kuandikisha kandarasi mpya la sivyo zikabiliwe na vikwazo.

Katika mahojiano na gazeti la Le Perisien waziri huyo wa maswala ya kigeni alisema: Tunahisi kwamba hatua ya kupita mipaka ya vikwazo hivyo haitakubalika. Raia wa Ulaya hawafai kuathirika na hatua ya Marekani kujiondoa katika makubaliano ambayo wao wenyewe walishiriki.

Alisema kuwa vikwazo hivyo vipya vitaathiri Marekani na Ulaya itaweka mikakati ya kulinda maslahi ya kampuni zake na kuanza kujadiliana na Washington kuhusu swala hilo.

Bwana Le Drian alisema kuwa uamuzi wa washirika wengine kuhusu makubaliano hayo ni lazima uheshimiwe.

Alisema kuwa athari za hatua hiyo ya Marekani tayari zimeanza kuhisiwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta na hali ya wasiwasi ya kisiasa katika eneo la mashariki ya kati.

Ufaransa, Uingereza na Ujerumani zote zimesema kuwa zitafanya kazi na Iran ili kujaribu kuokoa makubaliano hayo.

Waziri wa uchumi nchini Ujerumani Peter Altmaier amesema kuwa atafanya kazi na kampuni zilizoathiriwa ili kujaribu kupunguza madhara mabaya ya uamuzi huo wa Marekani.

No comments :

Post a Comment