Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 23, 2018

Afrika Kusini yamshukia Trump kuwaingilia kuhusu ardhi!

Afrika Kusini imemshutumu rais wa Marekani Donald Trump kwa kupanda mbegu za migawanyiko, baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa wizara yake ya mambo ya nchi za nje itachunguza hatua ya unyang'anyi wa ardhi na mashamba pamoja na madai ya mauaji ya wakulima kwa kiwango kikubwa nchini Afrika Kusini.Ujumbe wa Rais Donald Trump kwenye ukurasa wake wa Twitter, ulijiri baada ya taarifa iliyotangazwa katika kituo cha televisheni cha Fox News kuwa Afrika Kusini inapanga kubadilisha katiba yake. Ili kuharakisha hatua ya serikali kuchukua udhibiti wa ardhi na mashamba yanayomilikiwa na watu binafsi bila ya kuwafidia. Kama hatua ya kushughulikia suala la ukosefu wa usawa wa umiliki wa ardhi kwa msingi wa rangi.

Trump aliongeza kuwa amemtaka waziri wa mambo ya nchi za nje Mike Pompeo kuchunguza kwa makini hali ilivyo.

Ujumbe wa Trump ambao uliambatanisha ukurasa wa Twitter wa mtangazaji habari wa Fox News Tucker Carlson ulisema "serikali ya Afrika Kusini sasa inatwaa ardhi ya wazungu ambao ni wakulima”

Saa chache baadaye, serikali ya Afrika Kusini ilijibu kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa "Afrika Kusini inapinga kikamilifu, huu mtazamo finyu, unaolenga tu kuligawa taifa letu, na kutukumbusha kuhusu enzi za nyuma za ukoloni”

Wakati uchaguzi mkuu wa mwaka 2019 ukikaribia, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ameingilia kati kuharakisha mageuzi kuhusu umiliki wa ardhi, ili kuondoa dhuluma kuu za kihistoria dhidi ya Waafrika Kusini weusi ambao ndio wengi, kuanzia wakati wa ukoloni na utawala wa ubaguzi wa rangi uliomalizika 1994.

No comments :

Post a Comment