Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, August 9, 2018

Mazishi ya daktari bingwa yawaacha watu vinywa wazi!


MAZISHI ya Daktari Bingwa wa Saratani, Dk. Francis Mayaka, yamewaacha waombolezaji wilayani Muheza midomo wazi baada ya baba mdogo wa marehemu kuwakataza ndugu na jamaa kuaga mwili huo wala kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake.

Daktari huyo ambaye aliwahi kufanya kazi katika Hospitali ya Ocean Road ya jijini Dar es Salaam na baadaye kwenye hospitali za binafsi, alikufa kwa kujinyonga kwa kamba hivi karibuni nyumbani kwake katika kijiji cha Lusanga, wilayani Muheza na mpaka sasa chanzo cha kuchukua hatua hiyo hakijafahamika.

Baba mdogo wa marehemu, George Bakari, aliwatangazia waombelezaji kuwa mwili wa marehemu hautafunguliwa kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na hakuna mtu atakayeruhusiwa kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake.

Aidha, wasifu wa marehemu pia haukuruhisiwa kusomwa kwa waombolezaji hao.

Hatua hiyo iliwaduwaza waombolezaji waliojitokeza kwenye mazishi hayo huku wengi wakionekana kutoamini kinachoendelea kwa kuwa imekuwa desturi kwa mwili wa marehemu kuagwa na watu wa karibu na kuweka mashada ya maua kwenye kaburi lake.

Aidha, waombolezaji hao walishangazwa na uamuzi wa familia ya daktari huyo kuamua kumzika mbali na makaburi ya familia yake huku kaka wa marehemu, Raphael Mayaka akieleza hiyo ni kawaida kwa mtu anayekufa kwa kujinyonga.

Alisema kwa desturi na mila za Kabila la Kibondei, mtu akifa kwa kujinyonga hatakiwi kuzikwa katika makaburi ya familia kwa kuwa inaaminika kwa kufanya hivyo inaweza kusababisha watu wengine waendelee kufa kwa njia hiyo ya kujinyonga.

Alisema waliamua pia kuukata mwembe ambao marehemu alioutumia kujinyongea kando ya nyumba yake.

Raphael alisema kaka yake alikuwa daktari bingwa wa magonjwa ya saratani na aliwahi kufanya kazi nchini Urusi na baadaye Tanzania.

Naye mjomba wa marehemu, George Mayaka, alisema kabla ya tukio la  kujiua, daktari huyo alikuwa ametokea Dar es Salaam na kufika Muheza saa tano usiku.

Alisema alipofika walimuona akichukua kamba na ndoo na kwenda nayo pembeni ya nyumba ambayo kulikua na mwembe.

Alisema baadaye walishangaa kuona amechukua muda mrefu bila kurudi na walipomfuatilia walikuta tayari akiwa amekufa kwa kujinyonga kwa kamba kwenye mwembe huo.

Alisema marehemu ameacha mke mmoja mwenye asilia ya Kirusi na watoto saba.

Akiongoza ibada ya mazishi hayo, Mchungaji wa Kanisa la Anglikana Kijiji cha Lusanga, Kata ya Lusanga wilayani Muheza, Stuart Linza, aliwataka Wakristo wasimhukumu marehemu hata kama amekufa kwa kujinyonga.

No comments :

Post a Comment