Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameondoka kuelekea nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing nchini China, ambapo utafunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping. Katika mkutano huo Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli.
Mbali na kuhudhuria mkutano huo pia, Waziri Mkuu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni mbalimbali akiwemo Rais wa Kampuni ya CCECC, Rais wa Shirika la NORINCO, Rais wa Kampuni ya Zijin Gold Mine pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya saruji ya HEGNYA.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments :
Post a Comment