zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 21, 2018

Serikali ya Zanzibar yatoa kauli ajali ya MV Nyerere, watuma rambirambi!


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imetoa salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa wananchi wote walioguswa na ajali ya MV Nyerere iliyotokea jijini Mwanza jana .

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed akitoa taarifa ya Serikali leo Septemba 21,2018 amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali ya kivuko hicho iliyosababisha vifo vya baadhi ya wananchi.Amesema Serikali ya Zanzibar na watu wake wote wanaungana na ndugu wa Tanzania bara katika kipindi hiki kigumu kutokana na ajali hiyo.

"Kwa niaba ya Serikali, tuwatake wale wote walioguswa na ajali hiyo wawe wapole na wastahamilivu katika kipindi hiki kigumu" amesema.

Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Mwanasha Khamis akitoa taarifa za baraza hilo kwa niaba ya Spika amesema wajumbe wa baraza hilo wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za ajali hiyo.

Amesema msiba huo si wa wana Mwanza pekee bali ni wa Watanzania wote wakiwamo wajumbe wa baraza hilo kwa ujumla.

No comments :

Post a Comment