Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 18, 2018

Fatma Karume, LHRC na Alberto Msando wapinga vikali 'Umama'!


Msemo maarufu ulioibuka hivi karibuni wa 'Umama' umeifanya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kujitokeza hadharani na kupinga vikali kutumika ukidaiwa kuwa umelenga kufanya ubaguzi na udhalilishaji dhidi ya wanawake.

LHRC wametoa tamko lao hii leo ambapo wamesema matumizi ya neno hilo 'umama' ni muendelezo wa ubaguzi dhidi ya wanawake na kuongeza kuwa matumizi ya neno hilo yanalenga kuhalalisha dhana ya kwamba mwanamke ni dhaifu na hana uwezo wa kufanya mambo kwa ufanisi kama mwanaume.

Msemo huo umeshika kasi kwa siku za hivi karibuni ambapo baadhi ya sentensi ambazo zimekuwa zikitumika ni kama, " Mwanaume kubeba power bank ni umama, mwanaume anabeba Jenereta",.

Kwa upande wakili msomi nchini, Alberto Msando nae ameonekana kupinga vikali msemo huo wa 'umama' ambapo aliandika kupitia akaunti yake ya Instagram, " Aliyeanzisha huu utani (meme) wa ‘umama’ na wanaondelea nao nadhani wanasahau kwamba kama sio mama zetu basi tusingekuwa hapa tulipo. Ni upuuzi ni sentensi ambayo inamdhalilisha mwanamke. Kabla hujatunga sentensi na kutaka iwe ‘meme’ basi jiulize kama unaona aibu mama yako kuwa mama, utani huu unaonyesha ni jinsi gani bado ‘wanaume’ wanajiona wao ni bora kuliko wanawake".

Nae Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika TLS, Fatma Karume amepiga marufuku utumiaji wa neno hilo akisema kwamba ni udhalilishaji wa kumkandamiza mwanamke kupata haki zake.

Kufuatia tamko hilo la Kituo cha LHRC kukemea kutumika kwa neno hilo likitajwa kuwa ni udhalilishaji baadhi ya wananchi waliozungumza na Muungwana Blog walitaka wanaharakati hao kupinga vikali usemi wa 'wanaume wa Dar'.

No comments :

Post a Comment