Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 18, 2018

Vigogo wa juu wa Acacia wapandishwa kizimbani, wasomewa mashtaka 39!


Aliyekuwa makamu wa rais wa kampuni ya Acacia, Deo Mwanyika na Alex Lugendo ambaye ni mshauri wa Serikali ndani ya kampuni hiyo, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu mashtaka 39, yakiwemo ya utakatishaji fedha, kughushi na kula njama.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu  Mkazi  Mfawidhi,  Kevin Mhina na Jopo la mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili  wa  serikali  Mkuu,  Faraja Nchimbi  akisaidiana na Wakili wa serikali Mwandamizi,  Shadrack  Kimaro na Jackilline Nyantori.

Mbali na Mwanyika na Lugendo, washtakiwa wengine ni kampuni ya Mgodi ya Pangea, North Mara, Exploration na Bulyanhulu.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama 3, mashtaka yakughushi 7. Utakatishaji wa fedha 17, Kuwasilisha nyaraka  za uongo  kwa  Mamlaka ya Mapato Tanzanian (TRA), shtaka moja, kuongoza uhalifu wa kupangwa shtaka moja, kukwepa kodi, mashtaka 8 na shtaka moja la kutoa Rushwa.

Akisoma hati ya mashtaka wakili Nchimbi amedai washtakiwa hao pamoja na watu wengine ambao bado hawajakamatwa, walitenda makosa hayo kati ya Aprili 11.2008 na June 30.2007 katika sehemu tofauti za jiji la dar es Salaam, Kahama Mkoani Shinyanga, Tarime Mara, Biharamulo Kagera maeneo ambayo yapo katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini, Toronto Canada na nchini  Uingereza.

Imedaiwa katika kipindi hicho na mahali huko washtakiwa hao kwa pamoja wakiwa na watu wengine ambao bado hawajakamatwa walikula njama ya ya kutenda makosa ya kughushi na ukwepaji wa Kodi.

Pia mshtakiwa Mwanyika (56), na Lugendo (46), wanadaiwa kutoa msaada katika kusimamia mkakati wa kihalifu kwa nia ya kupata faida.

No comments :

Post a Comment