Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, October 25, 2018

Zanzibar kupewa ushirikiano kufanikisha shughuli ya utafutaji Mafuta!


MTAWALA wa Ras al Khaimah Shaikh Saud Bin Saqr Al Qasimi amemuhakikishia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa serikali yake itatoa ushirikiano katika kufanikisha shughuli ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kupitia Mkataba uliosainiwa hapo jana.

Shaikh Saud Bin Saqr Al Qasimi aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dk. Shein katika ukumbi wa Ikulu mjini Zanzibar, ambapo katika mazungumzo hayo Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd alihudhuria pamoja na viongozi wa Ras al Khaimah na wa Zanzibar.

Katika maelezo yake, Shaikh Al Qasimi alisifu juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Kampuni ya RAK GAS ya Ras al Khaimah katika kutekeleza mipango iliyopo ya utafutaji wa nishati hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Mtawala huyo alieleza kuvutiwa kwake na mipango inayoendelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sekta ya mafuta na gesi hasa kwa maamuzi yaliyofikiwa ya kutaka kujenga bandari maalum ya mafuta na gesi katika eneo la Mangapwani.

Nae Dk. Shein kwa upande wake alitumia fursa hiyo kwa kueleza juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ili kuimarisha ustawi wa wananchi.

Rais Dk. Shein alieleza kuwa mafanikio yanayoendelea kupatikana katika sekta ya utalii ambayo ni muhimili mkuu wa uchumi wa Zanzibar hivi sasa na kueleza azma na mikakati iliyowekwa ili kuongeza idadi ya watalii ifikapo mwaka 2020.

Aidha, Rais Dk. Shein alieleza mipango ya Zanzibar ya kujenga bandari maalum ya kusafirisha mafuta na gesi asilia kwa azma ya kurahisisha usafiri wa nishati hiyo ili kuondoa changamoto zilizopo hivi sasa za usafirishaji wa bidhaa pamoja na kujitayarisha na mipango ya hapo baadae.

Rais Dk. Shein alitoa shukurani kwa Mtawala huyo kwa kukubali kushirikiana na Zanzibar katika juhudi zake za kuimarisha sekta ya elimu, kwa kukubali kutoa nafasi maalum za masomo kwa wanafunzi wa Zanzibar katika nyanja mbali mbali zinazofundishwa katika vyuo vya Ras al Khaimah.

Shaikh Saud Bin Saqr Al Qasimi ameondoka nchini leo kurejea Ras al Khaimah ambapo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume aliagwa kwa heshima zote za Kitaifa pamoja na kuagwa na viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa  Haji Ussi Gavu.

No comments :

Post a Comment