Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 11, 2018

ASIMULIA ALIVYOBAKWA NA KUTOBOLEWA MACHO!

MKAZI wa Kijiji cha Nyambula, Kata ya Ngogwa, Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga, Fatuma Mabanga (50), amesimulia jinsi alivyobakwa na kutobolewa macho kisha kutelekezwa na mumewe.

Mabanga aliyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya Siku16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, yaliyofanyika wilayani Kahama.

Akisimulia mkasa huo, alisema ilikuwa Oktoba 28, 2014 wakati anatoka kwenye shughuli zake za biashara kwenda kumtembelea mdogo wake katika kijiji hicho na kukutana na mwanaume ambaye alimsalimia.

Alisema baada ya kusalimiana naye mwanamume huyo alimpiga mtama na kumkandamiza chini kwa nguvu na kumbaka kisha kupoteza fahamu na wakati anaamka siku inayofuata alijikuta hana uwezo wa kuona baada ya mbakaji huyo kumtoboa macho yote mawili.

Alisema wakati anahangaika bila kutambua wapi aelekee, walitokea wanafunzi wakamsaidia kumfikisha nyumbani kwake na kupelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Aliendelea kusimulia kuwa baada ya kupata ulemavu huo mume wake alimkimbia na kumwachia watoto 13 na kwenda kuoa mwanamke mwingine jirani na mahala anapoishi sasa.

Alisema kutokana na ulemavu wake Jeshi la Polisi Kitengo cha Dawati la Jinsia, Maendeleo ya Jamii na Ofisi za Ustawi wa Jamii, wamekuwa wakimhudumia kutokana na kutokuwa na uwezo wa kulima na kujihudumia mwenyewe.

Ofisa Ustawi wa Jamii, Abrahamani Nuru, alisema kuwa, Fatuma Mabanga, alikuwa na watoto 13 kati ya hao watatu walipoteza maisha, mmoja aliolewa na kuachika akiwa na watoto watatu na anaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi (VVU).

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Annamringi Macha, ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata mume wa mwanamke huyo na kumtaka atunze watoto wake badala ya kumwachia mkewe ambaye kwa sasa hana uwezo.

Alisema kuwa mbali na mtuhumiwa kufungwa miaka 17 baada ya kosa la kubaka na kumtoboa macho Fatuma, alisema ataomba mamlaka za juu kufanya upya tena mapitio ya kesi hiyo, ili aendelee kukaa jela kwa kuwa kitendo alichokifanya ni cha kinyama.

No comments :

Post a Comment