dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 11, 2018

Dk. Shein atarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano la Kimataifa la Kiswahili!

Kongamano la Pili la kimataifa la Kiswahili linatarajiwa kufanyika kesho katika ukumbi wa Sheikh Idrisa Abduliwakili kikwajuni mjini unguja huku wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mwenyekiti wa la Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) Dkt. Mohammed Seif Khatib amesema Kongamano hilo litakuwa na mijadala mbali mbali yenye lengo la kukuza, kuinua lugha ya Kiswahili duniani.

Alisema Mada zitakajadiliwa katika kongamno hilo fursa na changamoto mbali mbali zinazojitokeza katika Lugha ya Kiswahili hata hivyo alisema katika mkutano huo kutatoa fursa ya kubadiliashana uzoefu kwa wadau mbali mbali wa lugha ya Kiswahili.

 Alieleza kuwa kuwa zaidi ya watu 200 kutoka nchi mbalimbali watashiriki katika kongamano hilo ambapo mada mbalimbali za fasihi zitajadiliwa.

Alisema katika kongamano hilo pia Washiriki watapata fursa ya kulitatathmini kongamano lililopita mwaka jana na kuzinduwa kitabu cha Mtoto wa Mama kilichotungwa na mwandishi maarufu wa Riwaya Shafi Adam Shafi.

Aliongeza  kuwa Kongamano litatoa nafasi ya kuwatunza na kuwapa heshima Waandishi maarufu wa vitabu vya Riwaya na kutunukiwa Vyeti kwa mchango mkubwa walioutoa kwa jamii katika kutunga vitabu vyenye mantiki ya Kiswahili.

Aliwataja watakaopewa Vyeti kuwa ni pamoja na Marehemu Shafi Adam Shafi (KULI) Mohamed Said Abdalla (Bwana MSA), Mohamed Suleiman Mohamed (KIU na NYOTA YA REHEMA) na Said Ahmed Mohamed (ASALI CHUNGU).

“Hawa wote ni wazaliwa wa Zanzibar na tunaamini sisi kwamba ni waandishi bora wa riwaya ya Kiswahili Zanzibar na Baraza litawatunuku vyeti kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika uandishi”,alifahamisha Mwenyekiti huyo.

Aidha pia Baraza litawatunuku vyeti baadhi ya watunzi wa mashairi walioweka majina makubwa katika kukitunza Kiswahili  akiwemo bwana  Masauni Yussuf Masauni, marehemu Seif Salum, marehemu Bakar Abeid, marehemu Hijja Saleh Hijja na marehemu Idd Farahani.

Kongamano hilo ni la siku mbili ambalo litawashirikisha wataalamu, walimu na wanafunzi kutoka Kenya, Uganda, Burundi, Rwandwa, Nchi za Ulaya, Misri, Japan, Tanzania Bara na Australia.

No comments :

Post a Comment