Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi akimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bi.Halima Salum akielezea changamoto za kazi zinazoikabili Watendaji wa Hospitali ya Abdulaa Mzee Mkoani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Halima Salum akifafanua jambo wakati Balozi Seif alipofanya ziara kuangalia uwajibikaji wa Watendaji wa Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani.
Daktari Mkuu wa Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani Kisiwani Pemba Dr. Haji Mwita Haji akimtembeza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, wakati wa ziara yake kutembelea hospitali hiyo sehemu mbali mbali na kujionea changamoto zilizomo ndani yake.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balozi Seif Ali Iddi, akimjuilia hali Kijana Hassan Ali Hamadi Mkaazi wa Konde aliyelazwa katika Hospitali ya Abdulla Mzee Mkoani baada ya kupata ajali.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Na.Othman Khamis, OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Abdallah Mzee Mkoani kuangalia huduma za Afya zinazotolewa kwa Wananchi pamoja na kuona changamoto zinazowakabili watendaji wa Hospitali hiyo.
Balozi Seif aliuagiza Uongozi wa Hospitali hiyo kukaa na Afisa Mdhamini pamoja na Uongozi wa juu wa Wizara ya Afya kuainisha changamoto zinazowakabili ikiwemo vifaa vilivyoharibika ili Wizara izifanyie kazi.
Alisema haipendezi hata kidogo kuona kwamba Mshirika mkubwa wa Maendeleo ya Zanzibar Nchi ya China inajikita kusaidia gharama za uendelezaji miradi mbali mbali ikiwemo Hospitali na kutumia fedha za Walipa Kodi wake lakini muda mfupi baadae miradi hiyo inazorota au kufa kabisa.
Alisema vitendo kama hivyo vinapotokea mbali ya kuitia hasara kubwa Serikali pamoja na kuwakosesha huduma Wananchi lakini pia huwavunja moyo Washirika hao wanapoamua kusaidia Maendeleo.
No comments :
Post a Comment