Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 27, 2018

Sudan haitojisalimisha kwa yeyote - Rais Omar Al Bashir!

Rais wa Sudan Omar Al Bashir amesema mkwamo wa kiuchumi unaoikabaili nchi yake umesababiswa na vikwazo vya kiuchumi ilivyowekewa Sudan na mataifa ya magharibi.

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa la Sudan, Al Bashir akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Sheykh Mekki kilichopo katika jimbo la Al Jazeera alisema kuna taasisi na watu ambao wanahujumu maendeleo katika nchi.

Bashir alisema kwamba jamii inaunga mkono maendeleo na mfano wa wazi ni umati mkubwa waliohudhuria kwenye mkutano wake kufuatilia mazungumzo yake.

"Wanao haribu na kuchoma taasisi za nchi ni wahaini, majasusi na mamluki" alisema Bashir.Mkwamo wa uchumi uliopo Sudan unatokana na vikwazo vya uchumi ilivyowekewa na nchi za magharibi alisema rais Bashir na kuongeza kwamba.

" Wanafanya yote hayo ili tukawapigie magoti lakini kwa uwezo wa Allah hatutampigia magoti mtu yeyote. Hatutajisalimisha wala kuisamilisha nchi yetu kwa yeyote yule".

Polisi waliingilia kati maandamano yaliyofanyika Khartoum karibu na ikulu ya rais, Watu wanashikiliwa kutokana na maandamano hayo.

Kuhusiana na maandamano yanayoendelea nchini humo kupinga hali ya kiuchumi, rais jana Bashir alitoa maelezo " azimio la mabadiliko".

Wiki iliyopita maandamano yalianza katika miji ya Atbara na Port Sudan na siku ya Alhamisi yaliingia mjini Khartoum. Waandamanaji wanapinga kupanda kupita kiasi kwa thamani ya dola kitu kilichopelekea kupanda kwa bei ya mkate, nishati na kuleta hali ngumu ya kiuchumi.

Vyombo vya dola vimesema kwamba tangu maandamano hayo yaanze mnamo tarehe 19 Desemba mpaka hivi sasa watu 8 wamepoteza maisha, wakati kiongozi wa upinzani nchini humo Sadik Al Mahdi anasema idadi ya watu waliopoteza maisha ni 22.

Marekani ambayo ilianza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi mnamo mwaka 1997 kwa misingi ya kwamba nchi hiyo inahifadhi magaidi, iliahidi kuiondolea vikwazo Sudan ifikapo mwezi Januari.

No comments :

Post a Comment