Na. Thabit Madai, Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi CCM kimewataka wanachama wa chama hicho kutowachagua tena viongozi ndani ya chama hicho ambao wameshindwa kutekeleza ilani ya ccm ambayo inaelekeza namna ya kuwatatulia matatizo ya wananchi katika maeneo yao.Kimesema kuwarudisha viongozi hao walioshindwa kutekelza ilani ya chama hicho ni sawa na kuongeza mzigo pamoja na kurudisha nyuma jitihada za maendeleo ya taifa.
Akizungumza na Wananchi wakati wa halfa maalumu ya kukabidhi daraja kwa ajili ya kivuko, katika kijiji cha pangawe bondeni mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Amina Khamisi Keila alisema baadhi ya wabunge,wawakilishi na madiwani wameshindwa kutekeleza ahadi wanazozitoa katika maeneo yao jambo ambalo ni kinyume na maelekezo ya chama hicho.Alisema Viongozi kushindwa kutekeleza ilani kwa vitendo ikiwemo kuwatatulia wananchi matatizo ya maji safi na salama,ajira na vikundi vya ushirika wanapaswa kupigwa vita na kutopewa nena fursa ya kuongoza ifikapo 2020.
Aidha aliwapongeza viongozi wa jimbo la pangawe kwa kutekeleza ilani ya ccm kwa zaidi ya asilimia 85 katika jimbo ambalo limepelekea wananchi kuzidi kujenga ka sera za chama hicho.
Alisema Chama hicho kipo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi hivyo ni vyema kuwatumikia wananchi wao bila ubaguzi na kuwahamasisha wananchi kujiunga kwa wingi katika chama hicho ili kukizidishia ushindi katika uchaguzi mkuu wa mwa 2020.
Nae mwakilishi wa jimbo la Pangawe Khamis Juma Maalim alisema wameamua kujenga Daraja katika eneo la Pangawe Bondeni ili kuwaondoshea usumbufu wanaoupata wananchi wanaotumia njia hiyo na kuwaomba kulienzi na kulitunza ili liwe endelelevu na kufikia malengo yaliokusudiwa
No comments :
Post a Comment