Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 11, 2018

Umaskini wapunguzwa kwa asilimia 1 Rwanda!


Taasisi ya Taifa ya Takwimu Rwanda (NISR) imesema kiwango cha umasikini nchini humo kimepungua kwa asilimia moja.

Kutoka asilimia 39 kwa mwaka wa fedha 2013/2014 mpaka asilimia 38.2 kwa mwaka wa fedha 2016/2017.

Bodi ya NISR ilisema hayo katika uzinduzi wa utafiti wa tano wa hali ya maisha katika kaya (EICV5). Mkurugenzi Mkuu wa NISR, Yusuf Murangwa, alisema kushuka kwa umasikini kwa kiwango kidogo kumetokana na ukame ulioikumba nchi hiyo mwaka 2016 hivyo kuathiri mapato katika kilimo lakini uchumi wao umebaki kuwa imara.

Alisema ukame uliokithiri uliathiri uzalishaji wa mazao na kusababisha upungufu wa chakula na gharama za chakula kuongezeka mwaka jana.

Takwimu za utafiti huo zilichukuliwa kutoka sampuli ya kaya 14,580 zenye watu 64, 314 . Ilielezwa ingawa hali ya umasikini haijapungua kiasi kikubwa, hali ya maisha kwa wananchi wa Rwanda imeimarika kutokana na viashiria vya upatikanaji nishati ya umeme kuongezeka kutoka asilimia 22 hadi 34 ya kaya.

No comments :

Post a Comment