Dk. Shein aliyasema hayo Chimba, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba katika uzinduzi wa Skuli ya Msingi ya Chimba ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964.
Alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kutoa elimu bure na kuwataka wazazi wasitoe fedha kwa ajili ya matumizi ya ufagio na wala kununua chaki na badala yake kazi hiyo ni ya Wizara na Serikali itatoa gharamia gharama zote.
Alisema kuwa jambo hilo ni kubwa na Serikali itaendelea kugharamika kwa wananchi wake kwa kila hali na lisilobudi litafanywa na kusisitiza kuwa elimu haina mbadala.
Rais Dk. Shein aliwakata wazee kutochangia chochote na kama kuna mapungufu basi Serikali itafanya kazi wenyewe na wala sio wao.
Alisema kuwa elimu inatolewa bure kuanzia Chekechea, Msingi hadi Sekondari na kuwataka wananchi kuwaepuka wale wanaosema uongo kuhusu Serikali yao ambayo imekuwa ikiendelea kuimarisha sekta za maendeleo kila pembe ya Zanzibar.
Alieleza kuwa hadi mwisho wa mwaka jana uchumi wa Zanzibar umekuwa kwa asilimia 7.7 na sio kweli wale wanaosema kuwa uchumi wa Zanzibar umeanguka na kueleza kuwa kama ni hivyo Serikali isingeweza kutoa elimu zote bure.
No comments :
Post a Comment