Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akionesha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma leo wakati wa ziara yakukagua maendeleo ya ujenzi wa mji wa Serikali.
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora linalojengwa ndani ya mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma kama linavyoonekana ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika katika muda uliopangwa.
Mkadiriaji Majenzi kutoka Vikosi vya Ujenzi vya Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bi Selemina Rutambanzibwa akieleza hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa jengo la Wizara hiyo kwa Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe leo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo ya Wizara mbalimbali katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Dkt. Maulid Banyani akisisitiza jambo kwa Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe wakati wa ziara ya kukagua hatua iliyofikiwa katika majengo ya Wizara yanayojengwa na Shirika hilo katika mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma ikiwemo la Wizara ya Fedha na Mipango.
Katibu wa Kikosi Kazi cha Kuratibu Zoezi la Serikali Kuhamia Dodoma Bw. Meshach Bandawe (wakwanza kushoto) akishiriki kuchota mchanga unaotumika katika ujenzi wa jengo la Wizara ya fedha pamoja na mfundi wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) leo Jijini Dodoma wakati walipotembelea kujionea hatua iliyofikiwa.
(Picha na MAELEZO)
No comments :
Post a Comment