TUNDU LISSU HAS NOW BECOME A HOUSEHOLD NAME IN TANZANIA!
"CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
TAARIFA KWA UMMA- KUHUSU KAULI YA KUFEDHEHESHA ILIYOTOLEWA NA RAIS WA TFF
Kauli hii inapaswa kutazamwa kwa umakini mkubwa kwani imebeba ujumbe mahususi kuwa watu aina ya Tundu Lissu wanastahili kushughulikiwa kwenye sekta zote.
Kwetu sisi kama Chama ni Kuwa watu aina ya 'Tundu Lissu' na wenye 'U-Tundu Lissu' ni wale wote ambao wenye mtazamo na uwezo wa kuhoji, wanaotaka utawala wa sheria ufuatwe na wanaotaka sheria na Katiba ziheshimiwe na kuhakikisha kwamba kila mmoja anakuwa sawa mbele ya sheria na zaidi kila mwenye maoni na mawazo tofauti asikilizwe.
Sasa kauli ya Karia inatufanya tujiulize maswali mengi kama vile , inawezekana anawajua waliomshughulikia Tundu Lissu na ndio maana anataka kuwatumia kushughulikia 'Tundu Lissu' walioko kwenye mpira n.k.
Kutokana na kauli hii tunatafakari kuchukua hatua zifuatazo kama hataomba radhi;
1.Kusimamisha mahusiano na ushirikiano wowote na TFF ikiwemo kuwataka Wanachama wetu kutokushiriki matukio yote yanayoandaliwa na TFF.
2. Kususia bidhaa zote zenye nembo na au zinazotolewa na TFF zikiwemo jezi za timu za Taifa na nyinginezo.
3. Kuchukua hatua dhidi ya Makampuni ambayo yataendelea kushirikiana na TFF ikiwemo Kususia bidhaa zao, kwani watakuwa wanaunga mkono taasisi inayoongozwa kwa ubaguzi wa kisiasa.
4. Kuwashawishi wadau wa mpira kokote kusitisha mahusiano na TFF Kwani inaendeshwa kisiasa na kibaguzi.
Tunamtaka Ndugu Karia aombe radhi hadharani na aeleze UMMA kauli yake ilimaanisha nini na kama anaona ni haki kwa Lissu kupigwa risasi na ndio njia sahihi ya kushughulikia changamoto za kwenye Mpira.
John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje -CHADEMA
02 Februari, 2019"
No comments :
Post a Comment