Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, February 4, 2019

TUNDU LISSU AMSAMBARATISHA NDUGAI KATIKA MAJIBU YAKE!

SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA NDUGU NDUGAI AMBAE INAONESHA KAISHIWA KUHUSU LISSU!
TUNDU LISSU AMBAE ANAENDELEA KUITESA SERIKALI KATIKA ZIARA ZAKE UGHAIBUNI.

Njia ya mwongo huwa fupi sana. Mimi sijalipwa hata senti moja ya gharama za matibabu na Bunge. Hata senti moja. Shilingi milioni 43 ni michango ya hiari ya wabunge, sio fedha za Bunge kwa ajili ya matibabu yangu.


Nimechangiwa na maelfu ya watu wengine, Watanzania na wasio Watanzania. Hiyo ni michango ya hiari, sio haki ya kisheria ya Mbunge anayeumwa.

Milioni 203.7 zilizobaki ni mishahara na posho za kibunge ambazo kila Mbunge analipwa kila mwezi, awe anaumwa au mzima. Hizo nazo sio pesa za matibabu yangu.

Hata Spika Ndugai mwenyewe alipougua na kukaa India kwa zaidi ya miezi sita mwaka 2016, alilipwa mishahara na posho za kibunge, PAMOJA na pesa ya gharama za matibabu yake. (Yani Ndugai alilipiwa matibabu na bunge, akalipwa na stahiki zake zingine ikiwemo posho na mshahara kwa zaidi ya miezi 6 aliyokaa India).
_
Hivi ndivyo ambavyo imekuwa kwa kila Mbunge anayeumwa nchini mwetu (tangu uhuru), isipokuwa kwa Tundu Lissu aliyepigwa risasi 16 akiwa kazini Dodoma, katikati ya vikao vya Bunge.

Hata hivyo hizo milioni 203.7 abazotaja Ndugai ni malipo ya jumla kabla ya makato ya kodi ya mapato, makato mengine ya kisheria na makato ya mkopo wa gari. Makato haya hufanywa na Bunge moja kwa moja. Ukiondoa makato hayo, malipo yangu halisi hayafiki milioni 6 kwa mwezi.

Spika Ndugai anajitia aibu yeye mwenyewe na analiaibisha Bunge analoliongoza. Yeye mwenyewe alieleza bungeni mwezi Aprili mwaka jana kwamba Bunge haliwezi kulipia matibabu yangu kwa sababu:

1. Sikupata kibali cha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutibiwa nje ya nchi.

2. Katibu Mkuu Wizara ya Afya hajatoa kibali cha mimi kutibiwa nje.

3. Rais Magufuli hajatoa kibali cha kuidhinisha pesa za Bunge kutolewa kwa ajili ya matibabu yangu.

Leo Spika Ndugai anadai nimelipwa na bunge pesa ya gharama za matibabu yangu. Je, ni lini alipata vibali hivyo vitatu mpaka wanilipe fedha hizo? Hizi propaganda nyepesi ambazo hazimalizi hata masaa mawili kusambaratika. (Kwa aibu ameshajisambaratisha mwenyewe kwa kukanusha).!"

No comments :

Post a Comment