
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama Cha wananchi CUF waliokutana jijini Dar es salaam kuanzia March 12 mpaka March 15 katika mkutano mkuu wa chama hicho wamepitisha maazimio kulitaka baraza kuu la chama hicho taifa kuwafutia uanachama wanachama wote waliokisaliti chama hicho akiwemo katibu mkuu wa chama hicho MAALIM SEIF Sharif Hamad.
Wajumbe hao wamefikia maamuzi hayo Mara baada ya kuwachagua wajumbe 45 wa baraza kuu ambapo ni wajumbe 25 bara na 20 kutoka visiwani Zanzibar.
Akizungumza kupitisha maazimio hayo mwenyekiti wa CUF Taifa Prof Ibrahim LIPUMBA amesema kuwa amekubaliana na wajumbe hao na baraza kuu litawachukulia hatua Kali ikiwemo kuwafuta uanachama wale wote waliokisaliti chama hicho wakiongozwa na Maalim Seif .
"nasikia Maalim Seif kainunua ACT WAZALENDO na anataka kuhamia huko Sasa sisi tunamuambia tumemfukuza kabla hata hajaama"alisema Prof Lipumba.
Mkutano mkuu wa chama hicho umemalizika Leo jijini Dar es salaam
No comments :
Post a Comment