Namshukuru Mungu sana na wote waliotuombea tukiwa gerezani na tukatoka salama, sina imani kama waliotaka tukae magereza kama wamefurahia sisi kuendelea kuwa salama na afya njema mpaka sasa, unampeleka magereza mtu asiye na hatia huwezi kuwa na njema.
Unapompeleka mtu gerezani asiye na hatia ni kuvunja sheria, kumpeleka mtu asiye na hatia mahakamani alafu ukampeleka gerezani kwa kutumia mifumo ambayo kimsingi ni mifumo inayotakiwa itoe haki na kwa kutenda haki ni dhambi kwa Mungu pia ni kosa kisheria.
Hakimu, Waendesha mashtaka ofisi ya DPP na mamlaka ya tatu isiyojulikana inayounda utatu usio mtakatifu ndio unatumia sheria nafasi mamlaka vibaya kutesa watu kimwili na kifikra sio jambo jema kwa taifa letu.
Mahakama ya rufaa na Mahakama Kuu tunazishukuru kwa kuliona hili na kutoa maamuzi lakini maamuzi haya yametolewa baada ya siku 104/wiki 15/miezi mitatu nanusu na hiki ni kielelezo cha upungufu mkubwa wa mifumo yetu ya kutoa haki.
Ukienda kwenye magereza ukaona mateso wanayopata mahabusu utashangaa,katika mifumo yetu ya utoaji haki tunasema you are innocent until you are proven guilty, lakini kwa mfumo wa watu wanavyoishi katika magereza
yetu you are guilty before you are proven guilty.
Hatuna ugomvi na judiciary ya nchi yetu na udhaifu wa judiciary unasababishwa na udhaifu wa Serikali, ukubwa wa tatizo unaanzia polisi, sheria inawahitaji kuwe na mahabusu kwa saa zisizozidi 48, watu wanakuwa ndani hadi wiki 3-4 na zaidi. Watu wanakuwa subjected to torture wanateswa wanalazimishwa aidha wakiri makosa,nakubali ni mtindo unaotumiwa na polisi lakini ni wa kizamani hadi watu wanakuja kufika Mahakamani wameshateswa kweli,mfumo wetu wa utoaji haki unatakiwa kufanya kazi ya ziada sana.
Sijutii kuwa gerezani kwa siku 104, japo haikuwa halali lakini tumejifunza mambo mengi, na tutakuwa hatutendi haki kwa tuliyoyaona na kujifunza gerezani hatutayasema kwa sauti kubwa sana, tutayazungumza kwenye vyombo vya habari, Bungeni na mikutano ya hadhara.
Waandishi mnaofanya habari za kiuchunguzi fuatilieni muwapashe Watanzania na dunia wajue yanayoendelea katika magereza zetu, ni bahati mbaya sana magereza hawaruhusu kupiga picha na huenda wanaowahukumu watu waende magereza hawajawahi kufika magerezani waone.
Nimeandika mambo mengi nikiwa magereza nikasoma sheria ya magereza nikatambua kwamba nikitoa matamko lazima nipitie mguu wa magereza ili dunia ijue kwa hiyo nikashindwa kuvitoa nje ya magereza lakini nitatoa machachipisho mbalimbali ya nilichokiona magereza.
Nina ombi maalum kwa Jaji Mkuu kwa kuwa ndiye anamamlaka na Mahakama zote, vile vile ombi hili nalipeleka kwa IGP na watatu ni Kamishina wa magereza wafanye operesheni maalum waiite jina lolote lakini mimi ningependa waiite operesheni safisha magereza.
Neno upelelezi unaendelea limefanyika mwamvuli kutesa watu, neno hili linapokubaliwa kutumika mahakamani bila mipaka linapelekea watu kuozea magereza, wengine hawana hatia na hata wenye hatia basi muda wa upelelezi uwe na kikomo wasikamate watu ambao wajamaliza uchunguzi.
Baada ya muda fulani kama uchunguzi haujakamilika basi watu waachiwe, kuwaweka watu miaka 8, kuna kesi inaitwa ya ugaidi, tulikuwa tunaletwa na msafara unaitwa Special,chini ya ulinzi mkali tunachukukuliwa na Mh Matiko tunapelekwa Ukonga peke yetu tunaongezewa askari.
Tunachanganywa na wale watuhumiwa wa ugaidi tunapakiwa kwa ulinzi mkali, wakiletwa mahakamani Kisutu wanaingizwa moja kwa moja Mahakama Na. 1 haingii ndugu, waandishi wa habari wala mtu yoyote zaidi ya watu wa ulinzi na usalama.
Sababu tulikuwa tunaletwa nao hawa watuhumiwa wa ugaidi tulipata bahati ya kukaa nao na kuongea nao, wanaingizwa mahakama Na. 1 hakuna ndugu,mwandishi wa habari isipokuwa vyombo vya ulinzi na usalama, tunawapitia Ukonga tunachanganywa nao chini ya ulinzi mkali.
Hawa watuhumiwa wa ugaidi wamekaa magereza kati ya miaka 5-7 kila wakija Kisutu taarifa yao haitokei kwenye vyombo vya habari kwa sababu kesi zao zinaendeshwa kwa siri kwa ulinzi mkubwa, hakuna raia anaruhusiwa kuingia, sio ndugu, sio mwandishi wa habari wala mtu yoyote.
Tunachukuliwa peke yetu na Mhe Ester Matiko tunapelekwa Ukonga chini ya ulinzi mkali, tunafika Ukonga wanaongezeka askari wengine wengi chini ya ulinzi mkali wakikiita Kikosi Maalum (KM)
, tunachanganywa na wale watuhumiwa wa ugaidi tunapakiwa kwa ulinzi mkali, wakiletwa mahakamani Kisutu wanaingizwa moja kwa moja Mahakama Na. 1 haingii ndugu, waandishi wa habari wala mtu yoyote zaidi ya watu wa ulinzi na usalama.
Sababu tulikuwa tunaletwa nao hawa watuhumiwa wa ugaidi tulipata bahati ya kukaa nao na kuongea nao, wanaingizwa mahakama Na. 1 hakuna ndugu,mwandishi wa habari isipokuwa vyombo vya ulinzi na usalama, tunawapitia Ukonga tunachanganywa nao chini ya ulinzi mkali.
Hawa watuhumiwa wa ugaidi wamekaa magereza kati ya miaka 5-7 kila wakija Kisutu taarifa yao haitokei kwenye vyombo vya habari kwa sababu kesi zao zinaendeshwa kwa siri kwa ulinzi mkubwa, hakuna raia anaruhusiwa kuingia, sio ndugu, sio mwandishi wa habari wala mtu yoyote.
Hawa watuhumiwa wa ugaidi wamekaa ndani zaidi ya miaka 5, wanaambiwa uchunguzi unaendelea, wanalalamika wanasema wana familia, na wao ni binaadamu, wameacha wake na watoto, wako katika hali gani? hawajui, wanaishi mazingira mengine tofauti ndani ya magereza polisi.
As received
No comments :
Post a Comment