Mkenya Eliud Kipchoge ameshinda London Marathon kwa mara ya nne mfululizo huku Muingereza Mo Farah akimaliza wa tano.
Kipchoge 34, ambaye alivunja rekodi ya dunia ya mbio hizo mjini Berlin mwaka jana, alikamilisha mbio za leo kwa muda wa saa mbili dakika mbili na sekunde thalathini na nane (2: 02: 38.)
Waethiopia Mosinet Geremew na Mule Wasihun walimaliza katika nafasi ya pili na ya tatu nyuma ya Kipchoge, ambaye alikosa kuvunja rekodi yake mwenyewe ya Dunia kwa sekunde 59 ambayo ilikua 2:01:39.
Mkenya mwingine Brigid Kosgei, 25, alishinda mbio hizo upande wa kinadada na kuwa mwanamke wa kwanza wa umri mdogo kushinda London marathon upande wa wanawake.
Farah alimaliza mbio hizo dakika 3 na sekunde mojanyuma ya Kipchoge, huku Muingereza Callum Hawkins akimaliza katika nafasi ya 10.
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)

No comments :
Post a Comment