Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 24, 2019

Rais Duterte aiyambia Canada - "Ufilipino sio danguro"!

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameifokea nchi ya Canada kwa kushindwa kuchukua hatua juu ya takataka ilizosafirisha hadi katika nchi yake iliyopo kusini mashariki mwa Asia miaka kadhaa uliopita.

Nchi hiyo imewasilisha mara kadhaa malalamiko yake kupinga kidiplomasia hatua ya Canada ya kutuma tani za uchafu nchini Ufilipino kati ya mwaka 2013 na 2014.

Wiki hii Rais Duterte alitishia kurejesha takataka hizo nchini Canada, Canada inasema "ina nia sana "ya kutatua swala hilo na itashirikiana na Wafilipino kufanya hivyo.
Rais Duterte aliikosoa Canada juu ya mzozo huo wa muda mrefu wa kidiplomasia , akisema imeibadilisha nchi yake kuwa "danguro la kutupa uchafu".

Rais Duterte anafahamika kwa mtindo wake wa kutoa kaulli za wazi na mara nyingi hutumia lugha na kauli kali zenye utata.

No comments :

Post a Comment