Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, June 29, 2019

TUNDU LISSU - WATU WASIOJULIKANA WAJIHADHIRISHA!


ANAANDIKA MH. #TUNDU_LISSU.

Kuna siku nilisema hao wanaoitwa 'watu wasiojulikana' waliotaka kuniua watajidhihirisha tu. Sasa maneno hayo yametimia. 

Kwa maneno yake mwenyewe, Spika Ndugai alisema atakuja kuniangalia hospitalini Nairobi au kokote nitakapokuwa nimehamishiwa. Hakuja hospitalini Nairobi au Ubelgiji, lakini alikuwa anajua niko wapi kwa muda wote ambao nimekuwa nje ya Bunge. 

Mwezi Machi mwaka jana, Katibu wa Bunge alimwandikia barua kaka yangu, Wakili Alute Múghwai, kuhusu matibabu yangu. Barua hiyo ilinakiliwa kwangu nikiwa nimelazwa hospitalini UZ Leuven, na pia kwa Spika Ndugai. Kama Katibu wa Bunge alikuwa anajua niliko, Spika wa Bunge anawezaje kusema hajui niliko??? 

Nimelipwa mshahara na posho za kibunge tangu September 7 mpaka sasa, mwaka mmoja na miezi tisa. Sijawahi kuhudhuria kikao hata kimoja au mkutano mmoja wa Bunge katika kipindi hicho. Je, Bunge na Spika Ndugai walikuwa wananilipa mshahara na posho za kibunge bila kufahamu nilipo na sababu gani nipo huko??? Kweli??? 


Nikiwa hospitalini Nairobi nilitembelewa na Makamu wa Rais, Samia Suluh Hassan, aliyesema ametumwa na Rais Magufuli kuja kunijulia hali. Baada ya kuhamishiwa Ubelgiji nilitembelewa na Balozi wa Tanzania Ubelgiji. Kama, baada ya yote haya, Spika Ndugai bado hajui niliko basi ni shida kubwa. 

Lakini anachokisema Spika Ndugai sio cha ajabu. Hii ndiyo Tanzania ya Magufuli. Magufuli alimwambia Spika Ndugai atufukuze bungeni ili tushughulikiwe nje ya Bunge. Huu ndio utekelezaji wa maagizo ya Dikteta Uchwara. 

Nitarudi nyumbani September 7 kumkabili Dikteta Uchwara. Mimi ni Mtanzania na ni Mtanganyika. Hakuna mwenye mamlaka ya kunivua Utanganyika na Utanzania wangu. Nitarudi nyumbani September 7, regardless of what these cowards decide!!!

No comments :

Post a Comment