Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 13, 2019

CCM,CUF wakubaliana kugawana madaraka Kilwa!

Uongozi wa vyama vya siasa vikuu viwili vinavyounda Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Chama cha Mapinduzu(CCM) pamoja na Chama cha Wananchi (CUF) kwa pamoja wamekubaliana kugawana madaraka ya nafasi ya makamu mwenyekiti.

Nafasi hiyo ambayo kwa vipindi vinne vilivyopita ilikuwa ikiongozwa na madiwani kutoka chama cha wananchi- CUF sasa itaongozwa na diwani kutoka Chama cha mapinduzi CCM. Makubaliana hayo yamefikiwa baada ya mvutano wa siku nzima jambo lililopelekea wajumbe wa pande zote mbili kukutana ili kufikia muafaka baada ya idadi ya wajumbe kila upande  kulingana(17 kwa 17).
Baada ya wajumbe kurudi kwenye kikao 12 jioni,  mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Abou Musa Mjaka alisoma makubaliano hayo ambayo yaliridhiwa na pande zote mbili. Ambapo wawakilishi wa kila upande walisaini hati ya makubaliano.

Mbali na makubaliano hayo, lakini pia wajumbe wa baraza hilo (madiwani) walikubaliana kwamba kamati ya fedha itaongozwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Abou Mussa Mjaka (CUF), kamati ya UKIMWI (CM), kamati ya Mazingira(CUF ) na kamati ya Elimu ,Afya na huduma za jamii (CCM).

Kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 halmashauri ya wilaya ya Kilwa iliongozwa na CUF-Chama Cha Wananchi. Nikutokana na chama hicho kuwa na madiwani wengi kuliko wa Chama Cha Mapinduzi(CCM). Hata hivyo baadhi ya madiwani wa chama hicho walijiuzulu na kujiunga na CCM. Ambapo kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika, CCM kilishinda na kuongeza idadi ya madiwani wake.

No comments :

Post a Comment