Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametangaza kuongeza nafasi 60 badala ya 30 alizozitoa mwaka jana za udhamini wa masomo kwa wanafunzi bora wa Kidato cha Sita wenye viwango vya juu kabisa vya ufaulu.
Hayo aliyasema leo katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi bora wa Kidato cha Nne na cha Sita waliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa, hafla ya kuwapa zawadi maalum pamoja na chakula cha mchana alichowaandalia wanafunzi hao huko katika viwanja vya Ikulu mjini Zanzibar.
Rais Dk. Shein alisema kwamba idadi hiyo aliyoiongoza mwaka huu ni mara mbili ya nafasi za ufadhili wa masomo ambazo alizitoa mwaka jana kwa wanafunzi bora wa Kidato cha Sita.
Dk. Shein alieleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na utaratibu wa kuwapa udhamini wanafunzi bora wa Kidato cha Sita wenye viwango vya juu kabisa vya kufaulu kwa masomo ya sayansi na masomo ya sanaa.
Alifahamisha kuwa mwaka huu ameongeza nafasi hadi kufikia 60 badala ya 30 za mwaka jana kwani aliahidi kuendeleza utaratibu huo ili kupata wataalamu wa fani mbali mbali watakaoendelea na masomo yao ndani na nje.
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa wanafaunzi 187 waliofaulu kwa daraja la kwanza katika mtihani wa Kidato cha Nne mwaka jana pamoja na skuli bora kumi ambapo ufaulu wa mwaka jana ulikuwa ni wanafunzi 135
Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto. (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)


No comments :
Post a Comment