
Na Ahmad Mmow-Nachingwea.
Bei ya korosho zilizouzwa na kununuliwa leo katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI mkoani Lindi imeongezeka kwenye mnada huo nne uliofanyika mjini Nachingwea.
Katika mnada huo ambao barua 17 na maombi 77 yalisomwa, bei ya juu kwa kila kilo moja ni shilingi 2,812 ambapo bei ya chini ni shilingi 2,790.
Katika mnada huo uliofanyika katika viwanja vya RUNALI ni tani 2111.130 ndizo zilizouzwa na kununuliwa. Wakati mahitaji ya kampuni hizo 17 ni tani 13,967 na kilo 130.
Huku ikitajwa kwamba korosho nyingi zipo kwenye maghala AMCOS ambazo hazikufikishwa kwenye maghala makuu kutokana na changamoto ya vifungashio.
Katika ghala la umoja Liwale bei ya juu kwa kila kilo moja ni shilingi 2,803 na bei ya chini ni shilingi 2,790. Mahitaji ya wanunuzi katika ghala hilo yalikuwa tani 4748.22. Hata hivyo zilizoingizwa mnadani ni tani 770.22.
Katika ghala la Lindi farmers Nachingwea bei ya juu ni shilingi 2,812 na bei ya chini shilingi 2805. Katika ghala hilo la Lindi farmers mahitaji ya wanunuzi yalikuwa tani 3,708.500. Hata hivyo korosho zilizoingizwa sokoni ni tani 323.500 tu.
Aidha katika ghala la Naunambe Ruangwa bei ya juu ni shilingi 2,809 na bei ya chini ni shilingi 2805, wakati mahitaji ya wanunuzi kutoka kwenye ghala hilo yalikuwa ni tani tani 5510.608, hata hivyo korosho zilizoingizwa sokoni ni tani 1017.804
Katika mnada wa tatu bei ya juu kwa kila kilomoja ilikuwa shilingi 2,795. Hali ambayo inaonesha bei ya zao hilo kwa msimu wa 2019\2020 inapanda kila mnada.
No comments :
Post a Comment