Kiongozi wa kikosi cha walinzi wa mapinduzi cha jeshi la Iran, Jenerali Hossein Salami leo ameionya Marekani na washirika wake alipohutubia maandamano ya kuiungua mkono serikali na kuyapinga maandamano ya vurugu ya wiki iliyopita juu ya kupanda kwa bei ya mafuta.Akitumia matamshi sawa na ya maafisa wengine wa Iran, Jenerali Salami amezituhumu Marekani, Uingereza, Israel na Saudi Arabia kwa kuchochea machafuko ya wiki iliyopita.
Salami ameitumia hotuba hiyo kuyaonya mataifa ya Magharibi kuwa Iran itajibu kwa kuyaangamiza pindi yatavuka kile alichokiita kuwa ''Mstari mwekundu''.
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesema zaidi ya watu 100 waliuwawa wakati wa maandamano ya wiki iliyopita.
Iran inaandamwa na uchumi unaosuasua tangu Marekani iliporejesha vikwazo baada ya kujtioa kutoka mkataba wa nyuklia wa Iran na madola yenye nguvu wa mwaka 2015.
No comments :
Post a Comment