dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 24, 2019

Jeshi la Marekani lapoteza ndege isiyokuwa na rubani!

Jeshi la Marekani limesema kuwa limepoteza ndege isiyoendeshwa na rubani ambayo haikuwa na ulinzi katika mji mkuu wa Libya, Tripoli ambapo makundi hasimu yamekuwa yakipigania udhibiti wa mji huo kwa miezi kadhaa sasa.

Uongozi wa kijeshi wa Marekani barani Afrika (AFRICOM) umesema kuwa ndege hiyo isiyokuwa na rubani ilipotea ilipokuwa ikikadiria hali ya usalama na kufuatilia shughuli za makundi hayo yenye itikadi kali. Kikosi hicho cha AFRICOM hakikutoa sababu ya kupotea kwa ndege hiyo isiyokuwa na rubani lakini kimesema kuwa kinafanya uchunguzi.
Kimeongeza kuwa operesheni za ndege zisizokuwa na marubani nchini Libya, ''zimeshirikishwa vyema na maafisa wakuu wa serikali wanaostahili.'' Tangu mwaka 2015, Libya inatawaaliwa na serikali mbili, moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli na nyingine katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo.

Vikosi vya kijeshi vinavyoiunga mkono serikali ya Mashariki vimekuwa vikijaribu kuchukuwa udhibiti wa mji huo mkuu tangu mwezi Aprili.

No comments :

Post a Comment