dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 24, 2019

WATU 36 WAFARIKI KWA MAPOROMOKO YA UDONGO!


Mafisa nchini Kenya wamethibitisha kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na tukio la maporomoko ya udongo katika eneo la Pokot magharibi imefikia 36 .

Hii ni baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko iliyotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo hilo.

Maporomoko hayo yameathiri zaidi vijiji vya Nyarkulian na Parua, ambavyo vinasemekana kutenganishwa baada ya daraja kusombwa na.
Maafisa pia wamesema kuwa miili ya watu 12, ikiwemo ya watoto saba zilipatikana asubuhi ya Jumamosi.

Joel Bulal, mmoja wa wasimamizi wa serikali katika eneo hilo ameliambia gazeti la Daily Nation kuwa shughuli za uokozi zinaenedelea huku na kuwatafuta wale ambao hawajulikani waliko.

Kamishena wa jimbo hilo Apollo Okelo amesema watu wengine wengi huenda wamekwama chini ya matope na kuongeza kuwa shughuli ya kuwaokoa zinaathiriwana hali mbaya ya hewa.

"Tunajaribu kutafuta mahali ambapo daraja limesombwa na maji ya mafuriko,"alinukuliwa na mtando wa habari wa Standard nchini Kenya.

Licha ya tamko hilo la bwana Okello baadhi ya wanakijiji wanasema kinachoendelea kwa sasa ni ndege aini ya helikompta imekuwa ikizunguka katika eneo la tukio.

Picha zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zinaonesha miti iliyosombwa na maji na mingine kung'olewa, huku matope yakisambaa barabrani.

Katika Twitter yake, Shirika la Msalaba mwekundu limethibitisha ripoti zinazoashiria tukio la maporomoko "makubwa" ya matope.

Kumeshuhudiwa mvua nyingi katika eneo la Afrika Mashariki na upembe wa Afrika kwa wiki kadhaa sasa.

Kijiji kizima kimesombwa na maji nchi Sudan Kusini huku visa ajaliya maporomoko ya ardhi ikiripotiwa Tanzania, Ethiopia na Somalia.

Wanasayansi wanasema hali mbaya ya hewa inatarajiwa kukumba baadhi ya nchi katika kanda hiyo kwasababu viwango vya joto katika bahari Hindi vinatarajiwa kupanda kupita kiasi cha kawaida, hali ambayo huenda ikasababisha mvua kubwa.

No comments :

Post a Comment